BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAMICHEZO NAMNA WANAVYOPIGANA VIKUMBO SHIMIWI KUSAKA UBINGWA 2014/2015 KATIKA ARDHI YA MOROGORO.

Wanamichezo wa ofisi ya taifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali wakiwa katika maandamano wakati wakiingia katika uwanja wa jamhuri Morogoro katika ufunguzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ikishirikisha michezo mbalimbali yaaliyoanza kutimua vumbi jana mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.

KATIBA NA SHERIA YAANZA TAMBO SHIMIWI.
Na Mtanda Blog, Morogoro Sep 30/ 2014.
Timu ya soka ya wizara ya Katiba na Sheria Sport Club imeanza tambo baada ya kupata ushindi wao wa kwanza kwa kuigalagaza Ras Mbeya kwa bao 2-0 katika michezo inayoendelea yaShirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika uwanja wa Mazimbu mkoani Morogoro.



Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkoani hapa, Mwenyekiti wa wizara ya Katiba na Sheria Sport Club, Ephron Sanga alisema kuwa moto ulianza kuwashwa na vijana wake katika soka wataendeleza ubabe ili kuhakikisha timu inatinga hatua ya robo fainali na kuweka mikakati ya hatua ya robo fainali na fainali.



Mshambuliaji, Boniface Clement alianza kuiandikia wizara ya Katiba na Sheria Sport Club bao la kwanza dakika ya 22 kabla ya Nasour Mtimali akifunga la pili na ushindi kwenye dakika 50 na kuihakikishia timu yao kumaliza na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Ras Mbeya.


Sanga alisema kuwa kutokana na ushindi huo wa kwanza kwa upande wa soka umeanza kutoa milango ya neema kwa wizara hiyo ya kuona kila mchezo wataoshindana wanapata mafanikio makubwa na sio kuishia katika hatua za awali tu bali kufika fainali katika michezo ya soka, netiboli, karata, riadha, darts, kamba wanaume na wanawake ambayo wanaipigia hesabu ili zivuke katika hatua ya makundi.



“Tuna timu mzuri sana katika Shimiwi hii ya mwaka 2014, kwa upande wa soka tayari tumeanza vizuri kwa kuifumua Ras Mbeya kwa bao 2-0 huku kwenye kamba nako wanawake wakitamba vizuri tu kwa kupata ushindi lakini katika netiboli mpaka sasa tumepoteza michezo miwli, hivyo michezo iliyosalia tutajitahidi na tutafanya vizuri ili kupenya na kutinga hatua ya 16 bora.”alisema Sanga.


Katika michezo mingine ya soka Tamisemi ilitoshana nguvu na Ardhi kwa sare ya bao 1-1 wakati Ras Dar es Salaam iliibuka na ushindi waa bao 1-0 dhidi ya Mifugo na Habari yenyewe iliilaza Ras Simiyu kwa kuibanjua bao 2-0.



Michezo ya netibolo Ras Tanga iliigalagaza Viwanda kwa vikapu 51-8, Bunge ikipata ushindi vikapu 30-19 dhidi ya Ras Mara huku Ras Njombe ikiizabua Ras Tabora 37-7 wakati NFRA ilipata ushindi wa 35-9 kwa Mwanasheria Mkuu na Ukaguzi ikipoteza kwa GST 16-14.



Michezo ya kuvuta kamba wanawake timu ya wizara ya Katiba na Sheria Sport Club ilifanikiwa kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya NFRA, wakati Ikulu, Polisi, Ras Tabora wakipata ushindi wa 2-0 kwa Mambo ya Nje, Ras Njombe na Ras Kagera.



Kwa upande wa wanaume katika mchezo huo wa kuvuta kamba Hazina iliitambia Ras Katavi 2-0, huku Ikulu ikipata ushindi kwa Utumishi 2-0 wakati Wazziri Mkuu na Makamu wa Rais wakipata ushindi wa 2-0 mbele ya Uhamiaji na Ras Manyara.



RAS KATAVI YAIHENYESHA TIMU YA SOKA YA ULINZI SPORT CLUB SHIMIWI 2014.

Na Mtanda Blog, Morogoro. Sep 29/2014.

Timu ya soka ya Ras Katavi imeihenyesha timu ya Ulinzi Sport Club kwa kuibamiza bao 3-0katika michezo inayoendelea ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro



Mshambuliajia Michael Kasumbi alifunga mabao mawili katika dakika ya 39 na 50 huku Charles Jumanne akihitimisha kwa kufunga bao la tatu dakika ya 54.

Katika mchezo mungine timu ya soka ya Mahakama Sporti Clabu yenyewe iliiadhibu Mipango kwa kuitandika bao 2-0.



Washambuliaji Chilemba Chikawe alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 21 huku Thinei Muhazini akifunga bao la pili katika dakika 55 na kufanya Mipango kupoteza mbele ya Mahakama iliyoibuka na ushindi bao 2-0.



Katika mchezo wa netiboli NFRA ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi 35-9 michezo iliyofanyika asubuhi kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.


SHIMIWI YAANZA KUTIMUA VUMBI MOROGORO
Na Mtanda Blog/ Sep 28/2014.


Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) imeanza kutimua vumbi kwa kwa michezo ya ufunguzi huku timu ya soka ya wizara ya elimu ikishindwa kuitambia Ras Arusha kwa kulazimisha sare tasa ya 0-0 katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.



Wakati upande wa soka ukianza kwa sare tasa katika mchezo wa ufunguzi kwa netiboli mambo yalibadilika kwa Ikulu kuihenyesha Ras Morogoro kwa kuitandika vikapu 62-10 wakati mchezo wa kamba wanaume Mambo ya Nje ilikubali kupoteza mchezo mbele ya Ikulu huku RAS Iringa nayo ikifungwa kwa 1-0 dhidi ya Uchukuzi.



Katika michezo iliyofanyika leo (jana) timu ya soka ya Afya ilianza vyema kwa kuikung’uta Uhamiaji kwa bao 2-0 kutokana na mabao ya mshambuliaji Noel Mwalutende aliyepachika bao zote katika dakika ya 22 na 31.



Timu ya netiboli ya ofisi ya taifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali yenyewe ilianza mchezo wa kwanza kwa kutoa onyo baada ya kuisambaratisha Maendeleo ya jamii kwa vikapu 21-15 kutokana na kazi mzuri ya safu ya ufungaji inayoongozwa na Kabula Malale na Scola Stanslaus wakati Maendeleo ya jamii vikapu vyao vilifungwa na Rehema Mwingira na Pili Selemani.



Katika mchezo mungine timu ya netiboli ya habari, iliisambatisha Polisi kwa kuikandamiza vikapu 45-1 kazi mzuri ya Hadija Jaha na Johari Kachwamba wakati Polisi ikiongozwa na Elizaberth Sembuyage na Ajui Njoka waliambulia kufunga kikapu kimoja tu huku Tamisemi ikipata ushindi wa vikapu 48 mbele ya Ras Dar es Salaam.



Mchezo wa kuvuta kamba wanaume Ujenzi ilipata ushindi wa 2-0 kwa kuilaza Ras Tabora, Makamu wa Rais nayo ikipata ushindi wa 2-0 kwa kuitambia Ras Simiyu, Kilimo 2 NFRA 0, Ras Mbeya 2-0 Mambo ya Ndani, Uhamiaji 2-0 Tume ya Sheria, Sheria 1-1 GST.



Kwa upande wa kuvuta kamba wanawake Afya ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ras Tabora, Mifugo 1-0 Bunge, Kilimo 0-0 GST, Tamisemi 2-0 Sheria, Mambo ya Ndani 2-0 Ras Lindi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: