Mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond.
Uwepo wa maneno mengi yanayoongelewa juu ya uhusiano uliopo kati ya mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond’ na mrembo kutoka Uganda Zari Hassan ‘The boss Lady’, umezidi kuwapa maswali mashabiki wake. Wengi wao wamekuwa na hamu ya kutaka kujua ukweli juu ya hilo.
Maneno hayo yalisambaa kufuatia kuvuja kwa picha za wawili hao katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa kwenye mahaba mazito.
Jambo hilo limewapa shauku washabiki wake hao kutaka kujua, ikiwa kuna kinachoendelea baina ya mastaa hao, je, ni nini hatma ya penzi lake na membo Wema Sepetu (Miss Tanzania 2006)?
Licha ya kuenea kwa madai kuwa Wema na Diamond kwa sasa wameachana, bado wafuatiliaji wa mambo wanasema walipenda kufahamu ikiwa kuna ukweli wowote juu ya hilo?
Uwepo wa picha hizo kwenye mitandao umeongeza petroli kwenye moto uliokuwa ukiwaka juu ya uhusiano wa Wema na Diamond, kuwa mashakani kuvunjika.
Kufuatia mkanganyiko wa habari hizo, vyombo kadhaa vya habari vilikuwa vikimuwinda Diamond ili kufanya mahojiano naye, kupata ukweli juu ya tuhuma hizo zinazomuandama.
Katika mahojiano yake aliyofanya na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam, staa huyo anayetamba na wimbo wa ‘Nitampata wapi?’ amesema kuwa kwa sasa siyo muda mwafaka kuzungumzia masuala yanayohusu uhusiano wake.
“Kuna vitu vingi vinapokuja kuhusu mapenzi wakati mwingine inakuwa siyo vizuri kuvizungumzia. Kwani kuna vinavyofaa na visivyofaa kwenda kwenye vyombo vya habari.
Vitu vingi sana vinaandikwa na ninavisoma. Lakini ukweli ni kwamba, ni mimi na yeye (Wema), tunaoujua ukweli.
Gazeti la Taifa Leo la nchini Kenya, limemnukuu kupitia mahojiano aliyofanya na blog moja maarufu nchini likisema kuwa, staa huyo amekuwa na majibu nusunusu pale anapoulizwa kuhusu kadhia hiyo.
Katika mahojiano hayo aliulizwa kuwa inasemekana ameachwa na Wema kutokana na kutokuwa muaminifu katika mapenzi yao. Alichokijibu ndiyo kimezidisha maswali kwani alitoka na jibu moja tu ambalo ni “Sijui” lilisisitiza gazeti hilo.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wake, wakiongea na Starehe walisema kuwa, hali inaonyesha wazi kuwa kuna siri nzito baina ya mapenzi ya Wema na Diamond. Na ukitaka kulijua hilo, unaweza tu kuupitia wimbo wake aliouachia hivi karibuni wa ‘Nitampata wapi’.
Mbali ya ukakasi huo kushika chati bado kizunguzungu kinaendelea baada ya kuenea kwa picha za wawili hao wakiwa pamoja kimahaba, huku nyingine zikiwa na maneno chini yake ‘nadhani jibu la maswali yenu mmelipata’, yalisomeka baadhi ya maneno katika picha hizo kuashiria wawili hao wapo pamoja, ingawa hakuna aliyelizungumzia hilo.
“Ukiangalia maudhui ya wimbo ule, utagundua kuwa ndani ya akili ya Diamond kuna kitu kinamsumbua. Kwani ukiangalia historia ya maisha ya mastaa hao, utapata majibu sahihi na kuona kuwa kuna kinachoendelea” anasisitiza Joyce Mkoma (32) wa Dar es Salaam.
Tangu kuingia kwenye uhusiano mastaa Diamond na Wema wamekuwa wakikumbwa na misukosuko kadhaa iliyofikia hata kuwatenganisha kipindi fulani. Lakini hata hivyo baadaye walijipanga na kumaliza tofauti zao na kuendelea na maisha.
Hivyo ikiwa hilo linalosemekana litatokea, itakuwa si mara ya kwanza kutokea.
Starehe ilimtafuta staa huyo kutaka kujua undani juu ya tukio hilo, lakini hadi tunakwenda mitamboni simu ya yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ DIAMOND AMWEKA NJIA PANDA WEMA SAPETU, AELEKEZA AKILI KWA MREMBO ZARI HASSAN WA UGANDA ?, JIBU NDILO HILI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment