BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZITTO KABWE ATAJA BAADHI YA VIGOGO WALIOCHOTA FEDHA ZA ESCROW BUNGENI, WAZIRI MKUU NA ANDREW CHENGE WAJIWEKEA REKODI TANZANIA.

http://api.ning.com/files/DbrwTSp7ycPobKCl-EpCxsRTOlwGBOIdmi8v82N2B*B5dy7XVkJRq4D6T8eWQ2KyZ-AKF3YLxschi02TRvrKjOkvTm7YCv7f/zkwasanii2.jpgZitto Kabwe.

Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.

Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0QSKcabJ4sIcOIaZUxug0LARtCS__SKLhxQtfSmONY2nCeiIuVkPhSPxJVlVeOQKlenOvTmUlyjHnBqj5vQWBcCHuik6QA_yL_LtBcG1Zm9IzkXAJkTR_LLOxLXE6h9Qrjc2_mcKiaBQ/s400/PICHA+NA+1.JPG 

Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/12/PG4A0046.jpgWAZIRI MKUU MIZENGO PINDA.

Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi. 
MHE ANDREW CHENGE (MB).

Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: