BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK KIKWETE KUJENGA NYUMBA ZA ASKARI WANAJESHI 20,000 KABLA YA KUACHIA NGAZI KITI CHA URAIS 2015.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete akizungumza na mwanafunzi bora katika kozi ya maofisa wa Jeshi, Luteni Usu Engelbert Kessy muda mfupi baada ya Rais kutunuku kamisheni kwa maofisa wapya 171 wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli, Arusha juzi. (Picha na Freddy Maro).

RAIS Jakaya Kikwete ameahidi kuongeza idadi ya nyumba mpya zinazojengwa kwa ajili ya wanajeshi nchini kutoka 10,000 za sasa hadi 20,000 kabla ya kuondoka madarakani mwaka ujao.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama aliyasema hayo wilayani Monduli, Arusha wakati akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya 552 katika kambi ya Sokoine, mradi unaotekelezwa na kampuni ya China ya Shanghai Construction Group Limited.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUR_8ehcnQ0lERoYBFPxgSnGOy5wMG9fOJeSrBAI-GxFvBZ1CkZ_uay9BqooRPZTqmBJCWxaJbpgoZzcB61uqkZjB6hQvu7EafY0MxnMD2gchDmlzzS3PXHx26kIw3fjrlPC7CwKPT6Mkd/s1600/bangalo+2.jpg
Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi.

 Awali, Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi alifafanua kuwa Serikali ya watu wa China ilitoa mkopo wa Dola za Marekani milioni 300 (Sh bilioni 510) ambapo Serikali ya Tanzania ilichangia Dola milioni 15 (Sh bilioni 25.5) kati ya hizo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 6,064 kwa wanajeshi wenye familia.

Nyumba hizo kwa sasa zinajengwa kwenye mikoa tisa nchini ikiwemo ile ya Arusha, Pwani, Pemba, Dar es Salaam, Tanga, Kigoma, Dodoma, Kagera na Morogoro na tayari zaidi ya nyumba 2000 zimekwishakamilika.

Lakini, Rais Kikwete anaona kuwa nyumba 10,000 zinazojengwa sasa haziwezi kikidhi mahitaji yaliyopo pamoja na mpango wa kuwaondoa wanajeshi wote kutoka uraiani na kuwarudisha kambini, hivyo basi anatarajia kukutana na Balozi wa China nchini, wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kupata msaada zaidi kwa ujenzi wa nyumba zingine 10,000 ili kukamilisha idadi ya nyumba 20,000.

“Hakuna kiongozi yeyote anayeweza kupuuzia umuhimu wa kuwekeza katika Jeshi la Ulinzi na Serikali ya Tanzania imekuwa makini katika hili, maana mradi huu wa nyumba bora za kisasa kwa wanajeshi ulianza na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, nami nimeutekeleza kwa makini na sasa naanzisha ujenzi wa nyumba nyingine 10,000 ambazo zitakamilishwa na rais ajaye mwakani,” alisema Rais Kikwete.

Awali Rais Kikwete aliwatunuku nishani maofisa 171 waliohitimu mafunzo katika chuo cha mafunzo ya Kijeshi kilichopo wilayani Monduli na miongoni mwa wahitimu hao wanawake ni 15. Wengine ni maofisa wa jeshi kutoka nchi za Kenya (4), Rwanda (3) na Shelisheli (2).HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: