BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALIMU WAKUU 16 SHULE ZA MSINGI WASHUSHWA VYEO DODOMA.


“Ufaulu huu umeufanya mkoa kubaki katika rangi nyekundu za matokeo makubwa Sasa (BRN). Halmashauri zote zipo kwenye rangi nyekundu,”.PICHA|MAKTABA


Dodoma.
Walimu wakuu 16 wa shule za msingi mkoani hapa wameshushwa vyeo mwaka huu baada ya kushindwa kuwajibika vyema katika nafasi zao.


Hayo yalisemwa na Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda katika mkutano wa wadau wa elimu uliandaliwa kwa ajili ya kutangaza matokeo ya darasa la saba.


Kaponda aliwataja walimu wakuu hao wanatoka katika shule za Mwiyendaje, Dk. Samwel Malecela na Segara wilayani Chamwino.


Wengine walioshushwa vyeo ni walimu nane kutoka Wilaya ya Chemba ambao ni Makongoro, Konga, Hamia, Kubi, Ndoroboni, Chiole, Kidoga na Chinyika.


Walimu wakuu wengine ni waliokubwa katika kadhia hiyo ni wa shule za Kongogo, Mkakatika na Bankororo Wilaya ya Bahi.


Katika wilaya ya Mpwapwa walioshushwa vyeo ni walimu wakuu wa shule za Luhundiwa na Idiro.


Aidha, Kaponda alisema mkoa wa Dodoma ushika nafasi ya 21 kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wakati mwaka jana mkoa ulishika nafasi ya 23.


“Ufaulu huu umeufanya mkoa kubaki katika rangi nyekundu za matokeo makubwa Sasa (BRN). Halmashauri zote zipo kwenye rangi nyekundu,”alisema.


Hata hivyo, takwimu za ufaulu zinaonyesha hali ya matumaini kwamba ufaulu umekuwa ukipanda kwa miaka yote miwili licha ya ukweli kwamba kasi ya kupanda imekuwa ndogo,”alisema.


Kwa mujibu wa takwimu hizo kiwango cha ufaulu kwa mwaka jana kilikuwa ni asilimia 38.2 (sawa na wanafunzi 15,053), ambapo mwaka huu kimepanda na kufikia asilimia 45.3 (sawa na wanafunzi 16,672).MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: