Mwenyekiti mpya wa klabu ya Polisi Moro SC, Zuberi Chembera akipongezana na makamu mwenyekiti Odira Twew mara baada ya kuchaguzi kuongoza klabu hiyo katika uchaguzu wa kuchagua viongozi mbalimbali wa klabu hiyo katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro Desemba 20/ 2014.PICHA/MTANDA BLOG.
Kamanda wa polisi Morogoro, Leonard Paulo (katikati) akiwa na viongozi nafasi ya Mwenyekiti kushoto Zuber Chembera na makamu wake kulia Odira Tweve.
Wagombea wa nafasi mbalimbali wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya jumla.
Odira Tweve kushoto na Mwenyekti aliyemaliza muda wake, Issa Bushir wakijadiliana jambo baada ya kupiga kura awamu ya pili nafasi ya makamu mwenyekiti.
Kamati ya uchaguzi ukipiga hesabu kura awamu ya pili nafasi ya makamu mwenyekiti kabla ya kumtangaza mshindi.
Foleni ya askari wakielekea kupiga kura awamu ya pili kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Mgombea wa nafasi ya Makamwe Mwenyekiti, Juma Kalunga Wabwila akipiga kura awamu ya pili baada ya nafasi hiyo kushindwa kumpata mshindi.
Huyu ndiye mjumbe wa kwanza kupiga kura katika uchaguzi huo.
Kamanda wa jeshi la polisi Morogoro, Leonard Paulo akitumbukiza katarasi katika sanduku wakati upigaji kura.
Mshambuliaji wa zawani wa klabu ya Polisi Moro Sc, Fikiri Hussein akijaza karatasi kwa ajili kumchagua kiongozi anayemtaka katika uchaguzi huo.
Chembera akinadi sera na kuomba kura ili wajumbe wamchague kuwa mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro SC.
Njoki akinadi sera na kuomba kura ili wajumbe wamchague kuwa mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro SC.
Kaimu mkurugenzi wa sheria a wanachama kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF) Eliud Mvella akizungumza jambo wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali wa klabu ya Polisi Moro SC katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Mwenyekiti wa muda Issa Bushir aliyemaliza muda wake akitoa neno la shukrani kabla kujiuzuru ili kupisha uchaguzi ufanyike.
Baadhi ya wajumbe nao wakiwa katika mkutano huo.
Wagombe wa nafasi ya ujumbe kwa upande wa askari na raia wakifutilia matukio.
Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro namna unavyoonekana wakati wa uchaguzi huo.
Mwenyekiti na wasaidizi wake akionyeshaa karatasi za kupigia kura kuchagua wagombea nafasi mbambali.
Wajumbe waakifuatilia matukio.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Polisi Moro SC imepata viongozi mpya huku mkuu wa kituo cha Polisi Morogoro (OCD) akihemnyesha mpinzani wake katika nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi uliotawaliwa na figisufisu za ushindani wa hali ya juu uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Morogoro jana.
Mkuu wa kituo cha Polisi Morogoro (OCD), Zuberi Chembera ndiye aliyechaguliwa kwa kura 237 kuwa mwenyekiti mpya wa klabu hiyo baada ya kumshinda, Twahil Njoki aliyepata kura 37 ambaye kwa cheo yeye ni sajeti wa jeshi hilo.
Katika uchaguzi huo wajumbe walichagua viongozi mbalimbali wa klabu huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikiwatoa jasho wagombea kwa kushindwa kupata mshindi awamu ya kwanza na kulazimika kupigiwa kura kwa awamu ya pili ili kumpata mshindi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Aloyce Nyantora alisema kuwa klabu ya Polisi Moro SC imepata Mwenyekiti mpya, Zuberi Chembera ambaye amechaguliwa na wajumbe kwa kupata kura 237 huku mpinzani wake, Twahil Njoki akipata kura 37.
Nyantora alisema kuwa katika uchaguzi huo ulitawaliwa na upinzani wa hali ya juu hali iliyolazimika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti na wagombewa nafasi ya wajumbe askari kurudia kupigiwa kura kutakana na wagombea hao kushindwa kuvuka asilimia 50 ya kura zote.
“Ndugu wajumbe huu uchaguzi umekuwa na ushindani wa hali ya juu, nafasi ya Makamu Mwenyekiti tumeshindwa kumpata mshindi kutokana na wagombea wote kushindwa kupata kura zinazotosha kutangazwa mshindi na nafasi ya wagombea ujumbe upande wa askari wagombea wawili wamegongana kura hivyo kunarudia kupiga kura kuwachagua upya wagombea hao.”Alisema Nyantora.
Nyantora alieleza kuwa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti iligombea na wagombea watatu ambapo Odira Tweve yeye alipata kura 93 akifuatiwa na Juma Kalunga Wabwila aliyepata kura 81 huku Salum Juma Chuma akiambulia kura 74.
Odira Tweve na Kalunga Wabwila hawa wanalazimika kupigiwa kura kwa mara ya pili ili mmoja wao awe mshindi kwani kura walizopata hazitoshi kumtangaza mshindi Tweve kwani hajaweza kuvuka asilimia inaruhusu kupata ushindi huku Salum Chuma akiondoka katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kura chache alizopata awamu ya kwanza.Alisema Nyantora
Baada ya marudia ya uchaguzi huo, Odira Tweve alifanikiwa kumshinda mpinazni wake, Juma Wabwila kwa kupata kura 66 dhidi ya kura 43 ambapo idadi ya wajumbe waliopiga kura ikiwa 109, hali hiyo ilitokana na sehemu kubwa ya wajumbe kuondoka kurejea katika majukumu mengine ya kazi.
Kwa wajumbea askari waliogongana kwa kila mmoja kupata kura 129, Pascal Mwakabungu aliondoa kura moja na kumpigia Ramadhan Fumo ambaye alitangazwa mshindi kwa kupata kura 130 ambapo nafasi hiyo Kabunga Jindibu alipata kura 137 na Natali Ogha Bruno alipata kuwa 130 wakati wajumbe raia, Paulo Simkoko alipata ujumbe kwa kupata kura 192 huku Harry Mwambene akipata kura 163.
Katika uchaguzi huo ulihusisha wagombea askari katika nafasi ya Mwenyekiti na wajumbe askari huku raia ikichukua nafasi ya makamu mwenyekiti na wajumbe wawili ambapo jumla ya wajumbe 330 walijitokeza kujiandikisha kwa ajili ya kuchagua viongozi lakini idadi hiyo ilizidi kupungua kadri ya muda ulivyokuwa ukiendelea.
Upigaji wa kura ulianza majira ya saa 9:20 alasili ambapo wajumbe 272 ndiyo waliopiga kura awamu ya kwanza huku 58 wakishindwa kujitokeza kupiga kura, saa 9:35 alasili kura zilianza kuhesabiwa na zoezi kudumu kwa zaidi ya masaa mawili ambapo saa 12:08 jioni hiyo matokeo yalitangazwa lakini kutokana na nafasi ya makamu mwennyekiti na wajumbe askari, kura ilipigwa ili kupata washindi zoezi ambalo lilimalizika saa 1 usiku.

0 comments:
Post a Comment