Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amenusu kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la mlima Kitonga mkoani Iringa.
Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake, Kwame Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akielekeza namna ajali ilivyotokea.
“Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu tumepona.
Amesema pamoja na ajali hiyo kuonekana mbaya kwao, wanamshukuru Mungu kwani waliweza kutoka wakiwa salama na hakuna hata mmoja aliyepata maumivu makali.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment