BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIBONZO KILICHOCHORWA NA JARIDA LA CHARLE HEBDO JUU YA MTUME MOHMMED CHASABABISHA MAKANISA KUCHOMWA MOTO.

Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.

Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.

Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwaoMaandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed nchini Niger.

Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.

Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.

Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao.

Hawa ndiyo wandishi wa jarida la Charlie Hebdo ambao wamechapisha tena picha ya kibonzo cha mtume Muhammad.

Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe.

Msomaji akisoma Jarida la Charlie Hebdo amblo limewakera waisilamu kote duniani.

Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: