BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAJI YA MOTO ULIYOCHEMSHWA NA MWAKYEMBE WIZARA YA UCHUKUZI YATAZIDI KUWA YA MOTO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtAJu8ZwAVgf_XzBZNhGnTZTyb2mUC_V7kZU31zmh40XDRFUsAILSieqA89Ju2vDbXbmKOKH4eYkCt88k7luGaGkl3CPYiSNGgf4lhixAB7fWi-d0ZUAsp7mVPf9jSsD7d8q_Mi4pReT7i/s400/Samwel_Sitta.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema ataendelea kuwavalia njuga watu waliodhani kuwa maji yanapoa, baada ya Dk Harrison Mwakyembe kuondolewa katika wizara hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, yaliyofanyika hivi karibuni.


Sitta alisema hayo jana alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kukutana na sakata la wanawake wawili, waliokuwa wanataka kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja huo kuelekea Hong Kong.

Sitta aliagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya watumishi walioruhusu kupitishwa dawa za kulevya katika uwanja huo na kusisitiza kuwa waliokuwa wanadhani maji ya Mwakyembe yamepoa, wajue ndio kwanza yanazidi kuchemka.

“Wote watakaopatikana na na hatia ya kuwaruhusu Rehema Ndunguru na Moyo Ramadhani kupitisha dawa za kulevya aina ya heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wachukuliwe hatua mara moja,” alisema Sitta.

Alisema hatakubali hata kidogo Tanzania iwe ni uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya, hivyo kwa yeyote atakayehusika, asimamishwe kazi na kuwekwa ndani mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Wanawake hao walidai kuwa kila mmoja alikuwa amemeza kete 77 za heroin, mpaka kufikia jana mmoja alikuwa ametoa kete 78 na mwingine 73, polisi walikuwa wanaendelea kuwasimamia mpaka wahakikishe wametoa dawa zote.

Wanawake hao walidai kuwa kama wangefikisha mzigo huo sehemu husika, kila mmoja angelipwa dola 6.500 (sawa na Sh 11,700,000), ambapo wangepokelewa na tajiri wao ambaye hawajui jina lake, ila angewapigia simu.

“Rais na serikali yake hawataki Tanzania au kiwanja chochote cha ndege kupitisha dawa za kulevya… ni kosa kubwa. Lazima hao wanawake wataje wametumwa kwa sababu hawajui mtu ambaye angepokea mzigo huo,” alisema na kuongeza kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo. “Tutaendelea kuvalia njuga, waliodhani maji yanapoa baada ya Mwakyembe kubadilishwa wizara, hivi sasa ndiyo yanachemka,” Sitta alisema na kuongeza kuwa watumishi wa bandarini, kicheko chao kimeisha jana, la sivyo kitaisha leo atakapowatembelea.

Pia, alitembelea Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), na kusema kuwa serikali inatarajia kuondoa kikwazo cha sheria kinachokwamisha maendeleo.

Alisema zipo kampuni zenye shehena za mizigo ya shaba ambazo zinataka zipite Bandari ya Dar es Salaam, na reli hiyo ya Tazara.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: