Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akifafanua jambo wakati wa mikutano yake ya hadhara ya utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya miaka mitatu tangu kuchaguliwa mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu, katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Fire Manispaa ya Morogoro hivi karibuni. Picha Juma Mtanda.
Juma Mtanda, Morogoro.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdullaziz Abood amezitaka mamlaka zinazohusika, kuutafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro wa ardhi kati ya wafugaji na wakulima katika Bonde la Mgongola, wilayani Kilosa ili kuepuka umwagaji damu.
Rai hiyo imekuja wakati mkulima mmoja akiwa ameuawa usiku wa kuamikia Jumapili na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wa jamii ya Kimasai katika bonde hilo.
Watu wengine watano walijeruhiwa vibaya na sasa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leornad Paulo alimtaja marehemu kuwa ni Abdallah Shomari (27).
Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokwenda kuwajulia hali majeruhi hao jana, Abood alisema hali katika Bonde la Mgogola si shwari kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu.
Alisema kimsingi mgogoro kati ya makundi hayo ndani ya bonde hilo unazidi kukuwa na kwamba kuna haja kwa mamlaka zinazohusika, kuchukua hatua za haraka ili kurejesha amani.
Abood alisema Bonde la Mgongola linatumiwa na watanzania wengi kuendesha shughuli mbalimbali zikiwamo za kilimo na ufugaji na kwambao hao ni pamoja na wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
“Tuna taarifa za kuvamiwa na kushambuliwa kwa wakulima na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji, tayari mmoja amepoteza maisha. Tukio hili kwa upande wangu nalilaani vikali na halipendezi katika jamii ya wana Morogoro, navishauri vyombo vya dola kuwasaka na kuwachukulia hatua kali waliohusika,”alisema mbunge huyo.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Ruth Lyamuya alisema Januari 16 mwaka huu, hospitali hiyo ilipokea majeruhi watano waliotokana na ghasia zilizotokea Mgongola.
Dk Lyamuya aliwataja majeruhi hao kuwa ni pamoja na Mohamed Ramadhani (52), Radhaman Salum (81) na Rajabu Aly (45).
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
siasa
/ MBUNGE WA CCM AZITAKA MAMLAKA KUEPUSHA GHASIA ZA WAKULIMA NA WAFUGAJI, MGOGORO WA ARDHI MVOMERO MORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment