MWANABLOGU ACHARAZWA VIBOKO 1,000 HADHARANI, IKIWA SEHEMU YA KIFUNGO CHA MIAKA 10 JELA, KISA KUITUSI DINI.
Mwanablogu nchini Saudia amechapwa viboko hadharani kwa madai ya kutusi dini ya kiislamu.
Raif Badawi ambaye alianzisha mtandao kwa jina ''Liberal Saudi Network'' alihukumiwa kifungo cha miaka 10 msimu wa joto uliopita.
Mahakama pia iliagiza acharazwe viboko 1000.
Amechapwa viboko hivyo katika mji wa Jeddah.
Ilieleweka kwamba angetandikwa viboko hamsini na kwamba alitarajiwa kuchapwa viboko zaidi wiki zilizofuatia.
Mwanablogu huyo alichapwa viboko licha ya wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani kutaka kuondolewa kwa adhabu hiyo walioitaja kama ya kikatili.BBC
0 comments:
Post a Comment