PROFESA IBRAHIM LIPUMBA YAMKUTA YA KUMKUTA, ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI WAKIWEMO WAFUASI 32 JIJINI DAR ES SALAAM.
Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Tanzania.
Polisi Tanzania linamshikilia mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwemo wafuasi wake 32 pia kwa tuhuma za kufanya maandamano yanayodaiwa kuwa si halali.
Inadaiwa kuwa polisi hao awali walizuia maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kama sehemu ya maadhimisho ya kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso kwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Simon Siro ameiambia BBC kuwa wanamshikilia mwenyekiti huyo wa Chama cha siasa cha CUF na kwamba kati ya hao 32 wanaoshikiliwa wawili ni wanawake.
Polisi kwa mjibu wa Siro wanasema walikwisha waandikia barua barua viongozi wa chama hicho cha CUF kupinga kufanyika kwa maandamano hayo kwa sababu za kiusalama
Mwak 2001 chama cha CUF visiwani Zanzibar waliendesha maandamano yaliyosababisha baadhi ya Polisi na raia kadhaa kufa.
0 comments:
Post a Comment