BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI MAZINGIRA CHAKIFUNGIA KIWANDA CHA NGUO CHA 21st CENTURY KIHONDA MOROGORO.

http://www.itv.co.tz/media/image/Nemc%20moro%20still(1).jpg 
SEHEMU YA KIWANDA CHA NGUO CHA 21st CENTURY KILICHOPO KATA YA MAFISA KIHONDA MOROGORO.

 
Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa NEMC, Dk Robert Ntakamulenga.

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limekifungia kiwanda cha nguo cha 21st Century kilichopo eneo la Kihonda katika Manispaa ya Morogoro kufanya shughuli zozote za uzalishaji kuanzia jana, kutokana na kutiririsha maji taka na kusababisha uchafuzi wa mazingira.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa NEMC, Dk Robert Ntakamulenga alisema kiwanda hicho kina mitambo ya kutibu majitaka lakini haina uwezo wa kutibu majitaka hayo kufikia viwango vya mazingira vinavyotakiwa.

“Tangu mwaka 2006 Baraza na kwa nyakati tofauti na mamlaka nyingine zikiwemo za dola, wametoa maelekezo na amri mbalimbali kwa uongozi wa kiwanda hicho ili kuboresha mfumo wake wa kutibu majitaka yatokayo kiwandani humo kabla ya kuyaruhusu kuingia katika mabwawa ya kutibu majitaka yaliyokuwa yakimilikiwa na shirikisho la viwanda vya ngozi (TLAI) ambao sasa halipo, lakini kiwanda hicho kimeendelea kukaidi maagizo na maelekezo hayo hadi sasa,” alisema.

Alisema mabwawa ya kutibu majitaka yaliyokuwa yakimilikiwa na TLAI yalijengwa mahsusi kwa kutibu majitaka yatokanayo na viwanda vya ngozi na si majitaka yatokanayo na kiwanda cha nguo, kwani majitaka yatokanayo na kiwanda cha nguo yana kemikali na tindikali ambayo inaharibu mfumo wa ufanyaji kazi wa mabwawa hayo.

“Kutokana na hilo ni kwamba majitaka hayo sasa yanapita tu bila kusafishwa au kutibiwa na kuingia mto Ngerengere ambao nao unamwaga maji yake katika Mto Ruvu ambao ni chanzo kikubwa cha maji kwa matumizi mbalimbali wakiwemo wakazi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam,” alisema.

Alisema kutokana na kiwanda hicho kushindwa kurekebisha hali hiyo licha ya maelekezo waliyopewa, Baraza linaamini kwamba kuendelea kufanya kazi kwa kiwanda hicho kutasababisha athari kubwa kwa mazingira na afya ya wananchi ambao kwa namna moja au nyingine wanatumia maji ya mto Ngerengere.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: