Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza
kupiga kila raia na kusababisa kifo cha mama muuza Pombe za
kienyeji na kufariki dunia baada ya vurugu kuzuka katika mji mdogo wa Ilalu mkoani Iringa mapema leo.
Chanzo cha vurugu hizo kinaeleza kuwa kosa lilikuwa kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria.
Wananchi wamechoma magurudumu barabara Kuu ya Morogoro-Iringa na kusababisha magari kushindwa kutumia barabara hiyo huku Polisi
wakilazimika kukimbia baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi.
Baada ya tafrani hizi wananchi waliandamana na kwenda kuchoma moto kituo cha polisi.
Updated....
Baadaye gari tatu kutoka Iringa mjini zilizosheheni askari wa kutuliza ghasia (FFU) ziliwasili eneo hilo na kufyatua mabomu mfululizo kwa lengi la kutawanya wananchi na kuanza kuondoa uchafu uliokuwa umerundikwa barabarani kwa kusafisha na kuzima moto sanjari kutoa magurudumu barabarani.
Wananchi hao wamefanya uhalibifu kwa kuchoma moto magari mabovu yaliyoegeshwa katika kituo hicho.Chanzo http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/809267-vurugu-ilula-mwananchi-afariki-kituo-cha-polisi-chachomwa-moto.html
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ HABARI MPYA !!! VURUGU MJI MDOGO WA ILULA: MWANANCHI AFARIKI DUNIA HUKU KITUO CHA POLISI KIKICHOMWA MOTO IRINGA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment