BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IVORY COAST, GHANA ZATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA AFCON 2015.


Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeendelea katika michezo ya robo fainali kwa kushuhudia mchezo mmoja wa hatua hiyo ukizikutanisha Ghana pamoja na Guinea .

Katika Mchezo huo Ghana walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali wakiwachabanga Guinea kwa mabao 3-0.

Ghana walianza kazi mapema wakifumania nyavu za wapinzani wao mapema kwenye dakika ya nne kupitia kwa winga. Christian Atsu.

Black Stars walipata bao la pili kwenye kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Kwessi Appiah bao ambalo liliua matumaini ya Guinea .

Mwanzoni mwa kipindi cha pili Ghana walifunga bao la tatu mfungaji akiwa Christian Atsu tena na kuikatia timu yake tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali .

Timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni pamoja na wenyeji wa mashindano hayo Equatoarial Guinea, Ghana pamoja na Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo na
Ivory Coast.Timu ya taifa ya Ivory Coast imekuwa timu ya nne kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Algeria .

Ivory Coast imeifunga Algeria kwa matokeo ya 3-1 katika mchezo ambao ulimalizika ndani ya dakika 90 .

Mabao ya Ivory yalifungwa na Wilfred Bony ambaye alifunga mabao mawili huku Gervinho akifunga bao moja .

Bao pekee la Algeria lilifungwa na Hilal Soudani kwenye kipindi cha pili .

Katika mchezo wa nusu fainali Ivory Coast watachuana na Congo DRC wakati
wenyeji wa michuano hii Equatorial Guinea ikijipima ubavu na Ghana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: