BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA WILAYA AFURAHIA KUPATA UMAARUFU BAADA YA TUKIO LA KUFANYIWA FUJO JAJI JOSEPH WALIOBA.

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/makonda-vs-warioba.jpgMkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amesema tukio la kufanyiwa fujo aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, limempa umaarufu mkubwa na kumuwezesha kupata nafasi hiyo.


Alisema hayo alipohojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam, ambacho mtangazaji alitaka kujua kumekuwa na mazungumzo mengi kwenye mitandao ya kijamii ikielezea na kukosoa uteuzi wake.

http://1.bp.blogspot.com/-X-cf04JzZ4o/U-y0jL43smI/AAAAAAAC6r8/NvmC3Q0Mvv0/s640/0D6A4883.JPG
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.


 Makonda, ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka kundi la watu wenye malengo yanayofanana, alisema tukio hilo halijaathiri masuala yake ya kisiasa, badala yake limezidi kumpaisha.

“Kila tukio linaweza kuwa na mtazamo wa aina mbili negative (chanya) na positive (hasi). Mimi bahati mbaya najua kila tukio. Chochote kinachokuja mbele yangu ni sehemu ya kunisaidia mimi kusonga mbele,” alisema.

Alisema tukio la kufanyiwa fujo Jaji Warioba, lilimfanya kila mtu ndani na nje kumuulizia ili kumjua yeye (Makonda).

“Baada ya tukio lile, Tanzania hii na nje kila mtu alitaka kujua Paul Makonda ni nani, katokea wapi, anafanya nini, ni mtu wa namna gani, ana umbo gani? Lugha hiyo imesababisha mimi anione na kunitafuta na kupitia hivyo imempelekea kunifahamu na mimi nimemjua,” alisema Makonda.

Aliongeza: “Wale waliokuja kugundua ni propaganda za kitoto wanabaki tutakusaidia, wewe ni rafiki yetu, nimepata marafiki na napokea mawazo mengine.”

Novemba 3, mwaka huu, Jaji Warioba alifanyiwa fujo zilizosababisha kuvunjika kwa kongamano la kujadili mambo ya msingi ya kuangaliwa katika katiba inayopendekezwa, lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na wazungumzaji wakuu walikuwa ni waliokuwa wajumbe wa tume hiyo.

Wakati wa fujo hizo Makonda alionekana akimshika Jaji Warioba na ilidaiwa alimpiga. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: