BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NAMNA YA KUGUNDUA TATIZO LA MIMBA ILIYOTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI WA MWANAMKE NDIYO HUU.

https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xpa1/v/t1.0-9/s720x720/10919012_669373613173616_7164562023055684643_n.jpg?oh=467297c0edcd18e31b6d250ac583b497&oe=5520FBB7&__gda__=1433158993_e2adab1309c6f00a5fd7d9f51b65383bMimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni tatizo ambalo linaweza kumpata mwanamke yeyote na linapaswa kufahamika mapema ili hatua muafaka zichukuliwe.

Kwa kawaida mimba hutunga ndani ya mfuko wa kizazi isipokuwa mara chache huweza kutokea nje ya eneo hili maalumu.


Katika nyumba ya uzazi kuna mirija inayoitwa fallopian ambayo kazi yake ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji; ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi. Hapo ndipo mimba inapaswa kutokea.


Kwa bahati mbaya ama kutokana na hitilafu fulani mimba hiyo inaweza ikatungishiwa kwenye moja ya mirija miwili ya kizazi; upande wa kulia au kushoto.


Ikitokea hivyo, basi itafahamika kuwa mimba hiyo imetungwa nje ya kizazi. Vilevile mimba inaweza ikawa imetungwa nje ya nyumba ya uzazi au mirija. Asilimia 95 ya mimba zinazotungwa nje ya uterasi ama nyumba ya uzazi hutokea kwenye mirija hii ya fallopian.


Mimba zinazotungwa kwenye fallopian husababisha misuli inayozunguka mirija hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na mgandamizo wa mimba inavyokua. Hii husababisha mishipa inayopita karibu na fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema inasababisha madhara zaidi na hata kifo kwa mama.


Chanzo cha tatizo
Chanzo cha bado hakijajulikana, hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika mazingira ya kupata tatizo hili,.


Viashiria hivyo ni pamoja na magonjwa kama maambukizi katika mfumo wa uzazi hasa yale yanayosababisha uvimbe.


Vihatarishi vingine ni kama vile matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba au kuoteana kwa tishu za kwenye nyumba ya uzazi.


Mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi ni uvutaji wa sigara. Nikotini iliyoko ndani ya tumbaku huchochea kusinyaa kwa mirija ya ya fallopian na hata kusababisha mirija hiyo kuziba.


Jambo jingine ni upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani unaohusu mirija ya fallopian na kusababisha mrija husika kusinyaa.


Vilevile matumizi holela ya dawa zenye vichocheo (homoni) kama vile progesterone na clomiphene husababisha kupungua kwa uwezo wa fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye nyumba ya uzazi.


Magonjwa ya ngono ambayo yamekuwa ni moja ya chanzo cha tatizo hili ni kaswende au yale yanayosababisha ngozi nadini ya uzazi na mirija ya fallopian kuwa na uvimbe au umbo lisilo la kawaida kwa yai au kiinitete kusogea kwa wepesi.


Dalili za mimba nje ya uterasi
Mara nyingi dalili huanza kati ya wiki sita hadi nane baada ya mwanamke kuona hedhi kwa mara ya mwisho.


Mwanzoni mwa ujauzito hasa katika wiki ya ya kwanza, mimba iliyotunga nje ya mfuko wa kizazi huwa na dalili sawa ile iliyotungwa eneo la kawaida.


Hata hivyo ni vigumu kugundua mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa uzazi katika hatua za awali ingawa inaweza kuchochea kupata kichefuchefu na kuishiwa nguvu. Dalili hizi zinaweza kuwapata pia wale ambao mimba zimetungwa eneo la kawaida.


Hata hivyo, ni vyema mjamzito akaenda kliniki mapema angalao katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, ili kama ana tatizo hilo litatuliwe mapema.


Hii inatokana na ukweli kwamba akichelewa hadi ikifikia mimba ikifikia miezi sita hadi nane, utakuta tayari mirija ya uzazi imeshazidiwa.


Inakuwa haiwezi kuhimili kuubeba huu ujauzito, hivyo kumfanya mwanamke kupata maumivu makali chini ya nyonga, damu kutoka ukeni, kizunguzungu, kuzimia na shinikizo la damu kushuka.


Wakati mwingine maumivu huwepo kwenye mgongo mabega na shingo kwa kutegemeana na kiwango cha damu inayotoka kwenye mirija iliyopasuka kama ni nyingi sana.


Maumivu huweza kuwa makali kama kisu kina kata na yanaweza kuwa upande mmoja wa nyonga japokuwa si lazima yawe upande ulio na mimba


Jinsi ya kugundua
Daktari anaweza kubaini mjamzito ana tatizo la mimba nje ya uzazi kutokana na maelezo yake ya maumivu na viashiria vingine vinavyompata.


Vile vile daktari anaweza kumfanyia uchunguzi wa kawaida wa mwili. Vipimo mbalimbali vinaweza kuthibitisha hali hiyo kama kupima damu kwa aili ya kuangalia viwango vya vichocheo (homini) na kupima kiwango cha progesterone. Mama mwenye tatizo hilo, kiwango cha progesterone kina kuwa chini sana ukilinganisha na mama mwenye ujauzito uliotungwa eneo la kawaida.


Matibabu
Yako matibabu ya aina mbili; upasuaji ama kutumia dawa. Iwapo mirija itakuwa tayari imeshapasuka, upasuaji wa dharura hufanyika kwa ajili ya kuzuia kupoteza kwa damu zaidi.


Sehemu iliyopasuka huondolewa na mshipa wa damu uliopasuka hufungwa ili kuokoa maisha ya mama. Iwapo hali hiyo itabainika kabla ya mirija kupasuka, atapewa dawa ya kuharibu mimba.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: