BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHERIA MSUMENO: MKUU WA WILAYA YA MUFINDI APANDISHWA KIZIMBANI NA TAKUKURU.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu. Picha na Maktaba.

Mufindi.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu jana alifikishwa mahakamani pamoja na wakurugenzi wawili na maafisa wengine wawili wa halmashauri hiyo kujibu mashtaka ya kuingia mkataba wa ujenzi kinyume na Sheria ya manunuzi ya Umma na ya Takukuru.


Kesi hiyo Namba 1/2015 imefunguliwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Victoria Nongwa, na watuhumiwa wote walikana mashitaka yao.


Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni mkurugenzi wa zamani wa halmashauri hiyo, Limbakisye Shimwela ambaye kwa sasa anashikilia nafasi hiyo wilayani mikindani mkoani Mtwara, na mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo mkoani Kagera, Nasibu Bakari.


Watuhumiwa wengine waliofikishwa mahakama jana wakituhumiwa kufanya makosa hayo ni afisa mipango wa Halmashauri ya Mufindi, Cosmas Mduda na fundi ujenzi wa wilaya hiyo, Fedrick Zaveri.


Akisoma mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao, mwendesha mashitaka wa Takukuru mkoani Iringa, Imani Mizizi amedai kuwa kati ya Desemba 2010 na Februari 2011 watuhumiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la rushwa kinyume na kifungu cha 32 Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.


Katika shtaka la pili linalowakabili watu watatu katika kesi hiyo ambao ni Shimwela, Bakari na Cosmas, mwendesha mashtaka huyo wa Takukuru amedai kuwa watuhumiwa walitumia vibaya ofisi kinyume na kifungu cha 31 cha sheria hiyo ya Takukuru.


Watuhumiwa wote wamekana kosa na wameachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya kumtaka kila mmoja kuwa na wadhamani wawili na Sh1 milioni kwa kila mdhamini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: