SIMBA SC YAPAA HADI NAFASI YA NNE KUPITIA MGONGO WA POLISI MORO SC MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA.
Beki wa Polisi Moro SC, aNAF Seleman akichuana na mshambuliaji wa Simba Sc, Ibrahim Atib wakati wa ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro, Simba iliibuka na ushindi wa bao 2-0. PICHA JUMA MTANDA.
Morogoro. Simba imepaa hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuichapa Polisi Morogoro kwa mabao 2-0 jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Simba iliyokuwa ikishikiria nafasi ya tisa kabla ya mchezo huo ilipata bao lake la kwanza kupitia Ibrahimu Ajibu dakika ya 14, kabla ya Elius Maguri kupachika bao la pili dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 20, wakiwa nyuma kwa pointi tano kwa vinara Azam na Yanga na pointi moja kwa Kagera Sugar (21).
Simba ilianza mchezo kwa kasi na kuonekana kutawala katikati ya uwanja na kuwapa wakati mgumu wenyeji Polisi. Kasi ya Simba ilizaa matunda dakika ya 14, kwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Ibrahim Ajib akimalizia pasi ndefu ya Juuko Musheed.
Mchezaji wa Simba, Mohamed Hussein na Iman Mapunda wa Polisi Morogoro walinusurika kupewa kadi baada ya kutishia kupigana, lakini mwamuzi David Paul aliwaonya.
Simba ilipata pigo dakika ya 58, baada ya kipa wake Ivo Mapunda kuumia na kulazimika kutolewa nje nafasi yake kuchukuliwa na Peter Manyika. Ivo alipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Mshambuliaji Elius Maguri aliwainua mashabiki wa Simba dakika ya 63, kwa kupachika bao la pili akitumia vizuri uzembe wa kipa Tony Kavishe kushindwa kuweleana na mabeki wake.
Shinyanga: Kagera Sugar waliutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kuichapa JKT Ruvu kwa bao 1-0, shukrani wa goli la Atupele Green alilofunga dakika 31.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment