Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Azam FC imeshikwa sharti na Polisi Moro SC baada ya mchezo wao kumaliza kwa sare ya bao 2-2 katika uwanja wa jamhuri Morogoro.Hali hiyo iliwakuta tena klabu ya Simba SC baada ya kuvutwa sharubu na Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kwa kusalazimishwa sare tasa ya bao 0-0 huku Stend United nayo ikiambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.

0 comments:
Post a Comment