BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UPINZANI WA KISIASA: JULIUS MALEMA ACHAFUA HALI YA HEWA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LA AFRIKA YA KUSINI.


Julius Malema akiongea na waandishi wa habari baada ya kutolewa Bungeni.


Wabunge wenzake na Julius Malema wenye nguo nyekundu wakitolewa nje ya Bunge Afrika Kusini jana jioni February 12.

Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii Duniani kote iko, ukiyaona jana Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona hayo hata kwenye Mijengo ya Mabunge ya wenzetu yaani.

jana kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini, mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma wakati akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi zinazomkabili.

“Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.

Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema kutoka nje ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia na kumtoa kwa nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge, ambapo baadaye Rais Zuma aliendelea na hotuba yake.

Askari wa Bunge wakiwa nje ya Jengo la Bunge kuangalia usalama baada ya Wabunge hao kutolewa nje.

Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.

Hii ni video ya tukio la mwaka 2014.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: