BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANANCHI KUMBE HAWAJUI CHOCHOTE JUU YA UTENDAJI KAZI UKAGUZI HESABU ZA SERIKALI NA KAMATI YA ZITTO KABWE TANZANIA.


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad.

Dar es Salaam.
Wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya taasisi za Serikali za ukaguzi wa hesabu na jinsi zinavyofanya kazi ya kusimamia fedha za Umma, utafiti uliofanywa na Twaweza umebainisha.


Taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).


Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo jana, jijini Dar es Salaam, Mtafiti wa Twaweza, Constantine Manda amesema ni mwananchi mmoja tu kati ya watatu ameshawahi kusikia kuhusu CAG, na mtu mmoja tu kati ya sita anaweza kueleza shughuli za CAG.


Manda amesema mwananchi mmoja kati ya wanne amewahi kusikia kuhusu PAC na LAAC na mmoja kati ya kumi anaweza kuzielezea vema taasisi hizi. Aliongeza kuwa makundi ya wasomi, watu wenye kipato kikubwa na wanaume waliohojiwa ndiyo walionekana kuwa na taarifa zaidi kuhusu ofisi hizi.


“Wananchi wengi ambao hawazifahamu taasisi hizi hawakuweza kukumbuka mafanikio yoyote yaliyopatikana ndani ya ofisi hizo tatu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita,” alifafanua mtafiti huyo.


Katika utafiti huo, Twaweza iliwahoji watu 1,474 kwa njia ya simu, na kuwauliza maswali saba ili kupima uelewa wao wa masuala ya rushwa, taasisi za ukaguzi wa hesabu na usimamizi wa fedha za umma.


Wananchi waliulizwa kama wanaamini kuwa taasisi za ukaguzi wa hesabu ziko huru na kama wanaamini rushwa ipo Serikalini. Watu wawili kati ya watatu wamesema hawaamini kuwa taasisi za ukaguzi wa hesabu ziko huru.


Pia, wananchi tisa kati ya 10 wanaamini rushwa ipo Serikalini. Manda amesema wananchi hao wanaamini kuwa makampuni hutoa rushwa kwa viongozi wa serikali ili kushinda zabuni au mikataba.


Hata hivyo, Manda amesema asilimia 34 ya wananchi wanaamini kuwa aina hii ya rushwa huandikwa na kuonekana kwenye ripoti ya CAG.


“Watanzania wanaamini kuwa rushwa hairipotiwi kikamilifu kwa kiwango inachotendeka. Wengi wanapendekeza ripoti ya CAG kusambazwa kwenye redio kwa kuwa ndiyo njia yenye ufanisi zaidi,” ameongeza Manda.


Walipoulizwa nani anapaswa kuchukua hatua juu ya matokeo ya ripoti ya CAG, wananchi sita kati ya 10 wanatarajia Rais achukue hatua dhidi ya vitendo vya rushwa. Ni mwananchi mmoja tu kati ya 20 anaamini kuwa kamati za usimamizi PAC na LAAC zinatakiwa kuchukua hatua.


“Kadhalika, wananchi saba kati ya 10 wanatambua kuwa rushwa ni upotevu wa fedha zao. 



Tulitumia ripoti ya CAG ya mwaka 2012/13 kuelezea masuala ya ubadhilifu yaliyojitokeza, watu nane kati 10 wanaamini matukio hayo yanawaathiri kwa kiwango fulani,” ameeleza mtafiti huyo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: