BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ABIRIA TISA WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBILI NDANI YA HIFADHI YA MIKUMI MOROGORO.

Basi la Luwinzo linalofanya safari ya kusafirisha abiria kati ya Njombe na Dar es Salaam baada ya kupata ajali katika hifadhi ya Mikumi marchi 19/ 2015 kwa kugongana na basi ndogo la Msanga Line Express na kusababisha vifo vya watu saba kufariki dunia papo hapo na wengine 17 kujeruhiwa ikiwa ni siku mbili tu baada ya kutokea kwa ajali nyingine iliyohusisha basi la FM Safari na fuso marchi 17 mwaka huu, lenyewe likisababisha vifo vya watu wawili na abiria wanane kujeruhiwa mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
 

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumzia ajali iliyohusisha basi la Luwinzo kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam kugongana na basi ndogo la Msanga Line Express katika hifadhi ya Mikumi.
Hili ndilo basi ndogo mali ya Msanga Line Express baada ya kupata ajali.
HII ni ajali nyingine iliyotokea marchi 17 mwaka huu ndani ya hifadhi ya Mikumi ikihusisha basi la FM Safari na Fuso kugongana eneo la Mgoda katka hifadhi ya Mikumi ambapo ajali hii ilisababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi watu nane.
Basi la FM Safari baada ya kupata ajali.

Fuso likiwa linaonekana kwa nyumba baada ya kupinduka na kumwaga nyanya zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Ilula mkoani Iringa kwenda Dar es Salaam
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao akiwa katika eneo la tukio baada ya kutokea ajali hiyo.
 Sehemu ya mbele ya gari aina ya Fuso na basi la FM Safari zikionekana baada ya kupata ajali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: