Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni mwendo kasi uliochangiwa na dereva wa basi la FM Safari kushindwa kuwa makini wakati akiyapita magari mengine hali iliyolazimu kugongana uso kwa uso na fuso lililokuwa na dereva, abiria mmoja na utingo ambapo dereva na abiria walifariki dunia papo hapo huku utingo akijeruhiwa.
Dereva wa basi amevunjika mguu wa kushoto sambamba na mkono wa upande huo huku marejehi wengeni 18 kati yao wakikimbizwa kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na St Kizito.

0 comments:
Post a Comment