Ajali hiyo ni ya pili ndani ya siku mbili baada ya ajali nyingine katika hifadhi hiyo ikihusisha basi la FM Safari na Fuso kutokea marchi 17 majira ya saa 5:30 asubuhi na kusababisha watu wawili kufariki dunia na wengine nane kujeruhiwa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na utelezi ukichangiwa na mwendo kasi hali iliyomfanya dereva wa basi ndogo la Msanga Line Express kushindwa kulimudu vyema gari na kwenda kuligonga basi la Luwinzo lililokuwa likitokea Njombe kuelekea Dar es Salaam.
Kwa matukio ya picha za ajali hizo endelea kuungana nasi ili kuweza kuona matukio yote mawili ambayo yameghalimu maisha ya watu tisa na majeruhi 25.

0 comments:
Post a Comment