BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BWANA HARUSI AKOSA MKE SIKU YA HARUSI KISA KUSHINDWA KUJIBU SWALI LA HISABATI LA 15+6=17.

Harusi moja ilitibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli swali rahisi sana la hisibati aliloulizwa na bi harusi.
Kulingana na ripoti za walioshuhudia kihoja hicho cha aibu bi harusi anasemekana alimuuliza bwana harusi


''15 ukiongeza 6 utapata nini ''?

Polisi katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India wanasema kuwa sherehe za harusi hiyo zilitibuka baada ya bi harusi kufoka mumewe mtarajiwa alipotoa jibu lake . ''17 ''

Alikurupuka na kuondoka jukwaani akiwa amenuna akisema hawezi kuoa mtu ambaye hakwenda shuleni.

Juhudi zote za jamaa na marafiki waliofika kushuhudia nikaa hiyo ziliambulia patupu.
Bwana harusi alifeli swali la hisibati
 


Polisi katika jimbo hilo la Uttar Pradesh wanasema kuwa jamaa wa bwana na bi harusi wote walikubaliana kurejesheana zawadi zote walizokuwa wametoa kwaajili ya wapendwa hao.

Asilimia kubwa ya ndoa zote nchini India hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao.

Babake bi harusi Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha Rasoolabad aliiambia idhaa ya kihindi ya BBC kuwa mwanawe alishangaa kuwa mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa msomi.BBC

Mwezi uliopita bi harusi mwengine aliolewa na mgeni katika harusi yake baada ya Mumewe aliyekuwa amepanga kumuoa kuanguka kifaa dakika chache tu kabla ya wawili hao kuunganishwa kuwa mume na mke
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: