Na Hamida Shariff, Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete amesema moja ya mambo atakayojivunia baada ya kustaafu ni namna alivyotengeneza mazingira ya uwezeshwaji wa wanawake kujikwamua kiuchumi na kuondokana na mfumo kandamizi.
Kikwete alisema hayo juzi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa yalifanyika Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mabalozi kutoka nchi za Afrika na Umoja wa Mataifa.
Alisema amewapa wanawake fursa nyingi za nafasi za uongozi ili kuwe na uwakilishi mkubwa.
“Wanawake sasa ‘kazeni buti,’ msirudi nyuma...Katiba Inayopendekezwa imeweka bayana na inaeleza vizuri haki za wanawake ikiwamo ile ya usawa wa kijinsia yaani 50 kwa 50,” alisema Kikwete.
Aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura na kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba alisema kuwa Katiba inamtambua mtoto kuanzia umri wa siku moja hadi miaka 18. Wakati huohuo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahutubia mamia ya wanawake mkoani Dar es Salaam, huku akiwasisitiza kupigia kura ya ‘Ndiyo’ Katiba Inayopendekezwa.
“Kwa jinsi ulivyonieleza isingewezekana kulipwa pensheni. Ni lazima mifuko hii miwili (PSPF na NSSF) ilitakiwa ikae na kuoanisha michango na mamlaka inayowakutanisha ni SSRA,” alisema.
Dk Mosha alipoelezwa kwamba Waziri amemuomba aende Dar es Salaam kumuona, alisema kwa sasa hana hata nauli kwa vile kwa miaka yote 10 tangu amestaafu amekuwa akiishi maisha ya shida.
“Nitapata wapi nauli? Dar nimekanyagia mpaka nimechoka sasa hivi nina miaka 70 hiyo nguvu iko wapi? Miaka 10 nimeishi bila pensheni na kumbukumbu zangu zipo. Kabaka naomba nisaidie,”alisema.MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment