BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MOTO NAMNA ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WANAWAFUNZI WA KIKE "HOSTELI ZA MABIBO" DAR ES SALAAM.



Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakiangalia moja la bweni lililokuwa likiteketea jana katika hostel za Mabibo. Picha na Salihim Shao.

Dar es Salaam.
Jengo la ‘Block B’ la Hostel za Mabibo, za wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), jijini hapa limeungua kwa moto na kuteketeza vifaa na mali kadhaa za wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye jengo hilo.


Tukio hilo lililotokea leo majira ya 2:35 asubuhi linadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme katika jingo hilo.


Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa eneo la tukio akiahidi kubeba dhamana ya kushughulikia hasara ya mali, nyaraka na fedha kwa wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo.


“Kwanza kuhusu vyeti vilivyoungua ,tutashughulikia vipatikane vyote.Pili tutashughulikia hata bajeti za kujikimu kwa wale walioathirika, lakini pia kuanzia leo wanafunzi wote ambao walikuwa kwenye jengo hilo watahamishiwa jengo lingine wakati huo uchunguzi ukifanyika kufahamu chanzo cha moto,” alisema Profesa Mukandala.


Kwa upande wake, Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alitoa tahadhari ya usalama kwa mali za wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo huku akisisiza utulivu wakati uchunguzi wa chanzo hicho ukifanyika.



Taarifa kutoka miongoni mwa wanafunzi hao zimebainisha kuwa, wakati wa tukio hilo wanafunzi wawili wa kike waliruka kutoka gorofa ya pili mpaka chini na kujeruhiwa vibaya.


Askari wa Zima Moto walifika eneo la tukio hilo saa 3:45 asubuhi na kukuta moto ukiwa umeshapungua hatua iliyosababisha wanafunzi hao kuwashambulia huku wakiwazomea na kuwataka waondoke.


Viongozi wawili wa zima Moto, Omary Katonga kutoka Ilala na Mboke Msami wamesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni kutopata taarifa mapema.


“Moto umetokea saa 2:35 asubuhi kwa nini watujulishe tena kupitia Tanesco saa moja baadaye, tumefika hapa kwa kutumia dakika 23, wanakosea kutulaumu ila kinachotakiwa ni taarifa mapema,” amesema Katonga.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: