Klabu ya Yanga SC imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuilaza Kagera Sugar kwa kukusanya points 34 kufuatia michezo 17 ambapo mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Watani zao Simba SC imepokea kipigo kutoka kwa Mgambo JKT katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga huku Simba ikiambulia kipigo cha bao 2-0.
Yanga SC walipata mabao yao kupitia kwa Saimon Msuva aliyekwamisha mpira wavuni dakika ya 12 kwa njia ya penati huku bao la pili likiongezwa na mshambuliaji Amis Tamwe dakika ya 15 baada ya pasi murua ya Mrisho Ngassa huku Kagera Sugar ikipata bao lao kupitia mchezaji Sakum Kanoni kwa njia ya penalti.
Simba SC walikubali kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Mgambo JKT, mabao ya washindi walipachikwa wavuni na mshambuliaji Ally Nasoro dakika ya 21 huku Balimi Busungu akifunga bao la pili dakika ya 66 baada ya kipa wa Simba Ivo Mapunda kumchezea vibaya Full Mganga kabla ya kulimwa kadi nyekundu.
Mbeya City iliikandamiza Stend United bao 2-0 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

0 comments:
Post a Comment