BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAMWA KUBORESHA MRADI WA KUFUATILIA WAATHIRIKA WANAONYANYASWA NA UNYWAJI POMBE TANZANIA.


http://powermama.org/wp-content/uploads/2014/07/tamwa.jpg
 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kimekutana na Wahariri wa vyombo vya habari kutathimini, na kuangalia njia ya kuboresha mradi wa kufuatilia waathirika wanaonyanyaswa kutokana na matumizi ya pombe.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya majadiliano kuhusu mradi huo, Mratibu wa mradi, Gladiness Munuo, alisema mradi huo ulio na mwaka mmoja sasa, umefanikiwa kupokea kesi 107.

Munuuo alisema, kesi zilizowasilishwa ni 80 kutoka kwa wanawake wakiwashitaki waume zao, 20 kwa upande wa wanaume wakiwatuhumu wake zao, na saba ni kutoka kwa watoto kuwashitaki wazazi wao kutokana na matumizi mabaya ya pombe.

Kwa mujibu wa tafiti kutoka kata tatu zilizo katika wilaya ya Kinondoni, zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya vijana ndio wanaotumia matumizi ya pombe, na kuwadhuru wenza wao, kiasa cha kuwasababishia madhara mbalimbali.

“Mradi huu umelenga kubadilisha mfumo wa Watanzania kuhusu matumizi ya pombe kupita kiasi, kwani unahatarisha upatikanaji wa viongozi bora kwa siku zijazo,” alisema Munuo. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: