
Klabu ya Young Africans ya Tanzania imeiadhibu klabu ya Diamond Platnumz FC ya Zimbabwe kwa kuilaza bao 5-1 katika mchezo wa kombe la shirikisho katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambukliaji Mrisho Halfan Ngassa alipachika bao huku Haruna Niyonzima, Salum Telela na Amis Tambwe wakipachika kila mmoja bao moja moja.
Kiungo Salum Telela alifungua milango ya neema kwa Yanga SC kwa kufunga bao dakika ya 32 huku Haruna Niyonzima akipachika bao la pili dakika ya 43 huku Platnumz FC wakifunga bao pekee dakika ya 45 lilifungwa na Walter Musima.
Dakika ya 47 mshambuliaji Amisi Tambwe alifunga bao la tatu huku Mrisho Ngassa akigunga mara mbili katika dakika ya 55 na dakika ya 90 ya mchezo huo uliomalizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Platnumz FC.
Katika mchezo wa marudiano Platnumz FC kama itahitaji kusonga mbele italazimika kuifunga Yanga SC bao 4-0 katika mchezo utaofanyika nchini Zimbabwe wiki mbili zijazo.

0 comments:
Post a Comment