BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BREAKING NEWS !!! BASI NDOGO LILILOBEBA SIMBA UKAWA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA MAJERUHI 18 MORO.

Basi ndogo aina ya coaster lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Shinyanga limepata ajali eneo la Makunganya barabara kuu ya Dodoma-Morogoro na kusababisha watu watano kufariki dunia papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa mkoani Morogoro.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:40 jioni ilipata ajali hiyo baada ya utelezi uliosababishwa na kunyesha kwa mvua wakati mashabiki hao wakisafiri kwenda Shinyanga kusipa sapoti klabu yao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Kagera Sugar utaochezwa kesho kwenye uwanja wa Kambarage.

Maiti ya ajali hizo wamehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro sambamba na majeruhi hao 18 kupatiwa huduma ya kwanza.

Mwenyezi mungu awalaze roho za marehemu mahala pema peponi na kuwapa unafuu majeruhi wote katika ajali hiyo.
AMINA

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: