BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA HUKUMU KWA WANASIASA KUWA NI OKOTBA 25 MWAKA HUU.

 https://pbs.twimg.com/profile_images/1110813916/logo_SIASA.png

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imetangaza ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani ambapo utaanza rasmi agosti 21 mwaka huu nchini kote.


Kutokana na ratiba Tume hiyo imetoa tangazo kwa vyama vya siasa na wananchi kwa mamlaka waliopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35 (1), (3) (a) 37 (1) (a) na 46 (1) vya sheria ya taifa ya uchaguzi, sura ya 343, ratiba ya uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo.

Uteuzi wa wagombea ngazi ya urais, ubunge na udiwani kipenga kitaanza kupulizwa agosti 21 wakati kampeni ya uchaguzi ikitarajiwa kuanza rasmi agosti 22 huku siku maalumu ya kupiga kura ikitarajiwa kuwa oktoba 25 mwaka huu 2015.

tangazo hilo limetolewa chini ya mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji wa Rufaa Mstaafu Damian Lubuva Mei 23 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: