BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KANISA KATOLIKI LAJIONDOA KATIKA KUUNGA MKONO UCHAGUZU KUTOKANA NA MACHAFUKO BURUNDI


Muandamanaji aficha uso wake kwa majani Burundi.

Kanisa katoliki la Burundi limesema kuwa linajiondoa katika kuunga mkono uchaguzi unaotarajiwa nchini humo baada ya majuma kadhaa ya michafuko. 


 
Kanisa hilo limetoa taarifa Jumanne likisema kuwa limewasihi makisisi wote wanaohudumu kwenye tume za uchaguzi kujiondoa kwenye nyadhifa zao.

Jumatano serikali ya Burundi ilitoa wito kwa wa rundi kutoa michango yao ili kufadhili uchaguzi baada ya wafadhili wa kigeni kutishia kutofadhili iwapo rais Nkurunziza ataendelea na mpango wa kuwania wadhifa kwa muhula wa tatu.

Tangazo la rais mwishoni mwa mwezi uliopita limechochea ghasia na taharuki za kisiasa kwa majuma kadhaa ambapo zaidi ya watu 20 wamekufa na zaidi ya 500 kujeruhiwa kwenye makabiliano na polisi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: