KLABU YA POLISI MORO SC BADO INA HESABU KALI TU ZA KUBAKIA LIGI KUU MSIMU UJAO, ENDAPO MAMBO YATAKUWA HIVI LEO.
Kocha mkuu wa klabu ya Polisi Moro SC, John Tamba akiwa katika majukumu yake.
Juma Mtanda, Morogoro.
Kocha mkuu wa klabu ya Polisi Moro SC, John Tamba ameeleza kuwa timu yake inajindaa vyema kuhakikisha inapigana kiume hadi tone la mwisho, kwani kutokana na msimamo wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015 unaomalizika leo Mei 9 bado wanaona wana nafasi ya kubakia katika ligi hiyo licha ya kuburuza mkia.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Tamba alieleza kuwa kitu cha msingi kwao ni kupambana hadi tone la mwisho ili hesabu za nani atashuka daraja zitajulikana majira ya saa 12:15 jioni ya leo lakini hesabu za kubakia ligi kuu Tanzania bara bado zinawapa matumani kutokana na klabu tano kuwa katika janga la kushuka daraja msimu huu wa mwaka 2014/2015.
Tamba alisema kuwa ligi ya msimu huu ni ugumu na hiyo inatokana na ukweli kwamba kila klabu ilifanya maandalizi ya kutosha kukabiliana na mikimiki ya ligi hiyo kwani imekuwa na tofauti na ligi zilizopita.
“Kihesabu klabu ya Polisi Moro SC bado ina nafasi ya kubakia ligi kuu msimu ujao endapo katika mchezo wetu na Mbeya City tutapata matokeo mazuri ya ushindi huku tukiwaombea mabaya klabu nyingine nne kufanya vibaya katika michezo yao ya mwisho ifungwe ili sisi tupumue kwa kubaki ligi hii.”alisema Tamba.
Licha ya hayo kocha huyo ameoimba TFF kuwa makini na michezo ya leo kwani kuna kula dalili ya timu kupanga matokeo na kuepuka njama hizo klabu kupanga matokeo, wanapaswa kuwa waangalifu katika jambo hilo ambalo linaweza kujitokeza na kuiminya na kutoitendea haki mojawapo za klabu zenye kupigania kubaki ligi kuu msimu ujao.
Tamba alisema kuwa klabu tano mpaka sasa zinakabana koo kukwepa janga la kushuka daraja kutokana na msimamo wa ligi hiyo ulivyo.
Akielezea zaidi Tamba alisema kuwa Polisi Moro ina pointi 25 na endapo itashinda mchezo wake na Mbeya City leo Mei 9 itafikisha pointi 28 na kuziombea dua mbaya, Stend United, Mgambo JKT, Ndanda na Prison Tanzania zipoteze michezo yao ya mwisho ili wao kukwepa dhahama ya kushuka daraja kwani tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa yatawabeba Polisi Moro SC.
Kuanzia Stend United, Prison Tanzania, Mgambo JKT na Ndanda FC zina pointi 28 lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufungwa na kufunga zikikabana koo katika pointi hizo ambapo hesabu hizo zitatoa nafasi nani atabaki ligi kuu ama kushika kwani timu tano zitakuwa zimelingana pointi na hesabu ya bao za kufunga na kufungwa itatumika klabu kushuka ligi daraja la kwanza.
Kutokana na msimamo huo ili Polisi Moro iendelee kubaki ligi kuu msimu ujao italazimika iendelee kuziombea dua mbaya klabu hizo katika michezo ya mwisho ambapo Yanga SC itacheza na Ndanda, Azam FC ikichuana na Mgambo JKT huku Stend United ikicheze na Ruvu Shooting wakati Prison Tanzania ikicheza na Kagera Sugar.
Tamba alisema kuwa timu itayoshuka daraja itajulikana hasa saa 12:15 jioni baada ya kumalizika kwa michezo ya mwisho ya ligi hiyo na hapo itafahamika nani ameshuka daraja kati ya Ruvu Shooting, Stend United, Prison Tanzania, Ndanda, Polisi Moro SC na Mgambo JKT. Chanzo/MTANDA BLOG.
0 comments:
Post a Comment