KLABU YA RUVU SHOOTING YAUNGANA NA POLISI MORO SC KUSHUKA DARAJA LIGI KUU TANZANIA BARA MSIMU WA MWAKA 2014/2015.
Mgambo JKT.
Ndanda FC imefanikiwa kubaki ligi kuu Tanzania bara baada ya kuilaza Yanga SC bao 1-0 katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.
Kipigo walichopata Polisi Moro SC cha bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kimewafanya kupata tikiti ya kushuka daraja na kuungana na Ruvu Shooting.
Kwa upande wa Stend United yenyewe imepata matokeo mazuri ya bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kuinusuru timu hiyo kushuka daraja huku ikiiachia dhahama Ruvu Shooting.
Kikosi cha Prison.
Klabu za Polisi Moro SC na Ruvu Shooting zimefunga pazia la ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 kwa kushuka daraja baada ya kupata matokeo mabovu kwa kupoteza michezo yao.
Katika mchezo uliofanyika Mbeya iliwakutanisha timu ya Mbeya City dhidi ya Polisi Moro SC ambapo katika mchezo huo Mbeya City waliilaza Polisi Moro kwa bao 1-0.
Mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, kulikuwa na pambano kali na la kusisimua, ambapo Ndanda FC walikuwa wakiwakaribisha mabingwa wapya wa ligi hiyo Yanga SC na kuwabamiza Yanga bao 1-0 na kujihakikishia kubaki ligi kuu.
Matokeo hayo yalizua shangwe na vifijo kwa Ndanda baada ya kijihakikishia nafsi yao ya kubaki ligi kuu kwani endapo kama wangefungwa katika mchezo huo basi Ndanda walikuwa wanashuka daraja moja kwa moja.
Katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika pale Stand United walipokuwa wanawakaribisha Ruvu Shooting ambapo katika matokeo ya mechi hiyo Stand waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kujinusuru na janga la kushuka daraja, huku Ruvu Shooting wao wakiteremka rasmi daraja.
Kwenye uwanja wa Manungu Complex Turiani, Mtibwa walitoshana nguvu na Coastal Union kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 ambapo katika mchezo huo hakuna timu iliyotetereka na matokeo hayo.
Klabu ya Prisons ya Mbeya na Kagera Sugar hawakuweza kufumania nyavu na kumaliza mchezo huo sare ya 0-0 ulipigwa dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza huku matokeo hayo yakitoa faida kwa Prisons kujinusuru na kushuka daraja
Simba ilifanikiwa kuibuka na ushinda wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu JKT wakati katika uwanja wa Chamazi Complex, Azam FC na Mgambo JKT nazo zilimaliza mchezo wao kwa sate tasa ya 0-0.
Timu ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu ujao ni Mwadui FC, Majimaji, Toto Africans na African Sports.
0 comments:
Post a Comment