Nukuu za Lowassa kwenye Safari yake ya Matumaini, leo jijini Arusha:
Leo nimewaita hapa ili kutangaza nia ya kugombea Urais, je mtanipa ?
Mara ya kwanza niligombea Urais mwaka 1995, mara ya pili ilikuwa mwaka 2005 lakini nlimuunga mkono Kikwete. Na mimi ndo nilikuwa mwenyekiti wa Kampeni.
- Kilichonifanya nitangaze nia ni hali tete katika nchi yetu.
Moja ni kisiasa:
- Nataka nijenge siasa mpya na kuacha siasa mfilisi ambazo zimejaa chuki wa kila aina.
Uchumi wa nchi:
- Vijana wanataka kuona wanapata ajira, Mikopo.
- Watanzania wanaendelea kuamini kwamba wanaweza pata mabadiliko ndani ya CCM. Nyerere alisema Watanzania wasipopata mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.
- Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya maamuzi magumu
- Mabadiliko yanataka uongozi makini thabiti na usio yumba. Uongozi wenye ubunifu na upeo mkubwa. uongozi unaoamini katika shirikisho katika ujenzi. Uongozi unaozingatia muda
- Angalia, kushangilia kwenu kusimpe sababu ya Mangula Kunishughulikia
- Unapomtafuta Rais ni kutafuta Amiri Jeshi Mkuu, ni kumtafuta mwenyekiti wa CCM. naamini vigenzo hivyo ninavyo na nilishiriki vita vya Kagera nikiwa kiongozi wa mbele kwenye vita ya Idd Amin. Waulize wengine, walifika Kagera? Hiyo ndo safari ya matumaini
Dira:
- Kuimalisha Muungano wetu
- Kushughulikia mambo ya kibaguzi na kikabila
- Kusimamia uchumi
- Kuondokana na sifa mbaya ya Taifa lenye mfumo wa kuombaomba.
- Kujenga mfumo mpya wa Elimu
Hayo niloyaeleza ndio yatakuwa msingi wangu wa kuongoza nchi.
- Marais waliotangulia wamefanya kazi kubwa sana lakini kuna nafasi ya kufanya zaidi yao.
- Nimeamua kugombea ili kupambana na umasikini. Tuna Rasilimali nyingi sana
- Uongozi wangu utakuwa mwanzo wa mchakamchaka wa Maendeleo.
- Nitaimalisha misingi ya Muungano na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar. Kujenga Uzalendo, Uadilifu na Kumaliza rushwa.
- Tumekuwa wajuzi wa kutunga sera bila kuzifanyia kazi. Sera inatungwa Tanzania, inaenda Uganda inahaririwa na Kenya na Uganda wanaifanyia kazi. Mimi ntasimamia sera
- Nitadumisha Uraia Mwema.
- Nitafanya maamuzi magumu kila inapotakiwa
- Nitaleta mapinduzi ya Viwanda
- Nitakabiliana na Rushwa kwa vitendo siyo maneno
- Nitaboresha Masirahi ya Walimu na wafanyakazi wa Sekta ya Umma.
- Nitaboresha huduma za afya, maji safi na salama.
- Ntawawekea utaratibu mzuri wa Bodaboda, Mama Ntilie, Machinga hawatafukuzwa barabarani.
- Kwenye Michezo tumechoka kuwa Kichwa cha mwenda wazimu na washiriki washindwa.
- Kazi yangu ya kwanza itakua kukabiliana na msongamano na ndani ya miezi 12 itakuwa Historia
- Nauchukia umasikini
- Tuanze pamoja mchakato wa maendeleo. Hii Ndo Safari ya maendeleo.
- Mungu Ibariki Tanzania Mungu, Ibariki Afrika Asanteni sana…
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment