Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick
amezipongeza mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam,
kwa mvua hizo kuisaidia serikali katika utekelezaji wa hukumu ya
mahakama kuu, kuwaamuru wakazi wa mabondeni kuhama kwa lazima.
Wananchi
waligoma katakata kuhama huku serikali ikijishauri namna
ya kuwahamisha watu kwa nguvu bila kuleta madhara, haswa kwa kuzingatia mwaka huu ni wa uchaguzi.
Mvua hizo zinazoendelea kunyesha na zimeisaidia
serikali kwa kiasi kikubwa kuwahamisha wananchi hao.
Mkuu huyo wa Mkoa, ametoa shukrani hizo, katika mahojiano ya moja kwa
moja katika kipindi cha Kumepambazika, kinachorushwa na Redio One Stereo
asubuhi leo.
Alisema kuwa imetokea taarifa za kupoteza maisha kwa watu wengine wawili,
mmoja akisombwa na maji wakati alipotaka kuvuka mto Ng'ombe na kumzidi nguvu na
kumsomba wakati mwingine ni mtoto mdogo wa miaka miwili aliyekuwa akicheza
nje ya nyumba yao ambapo maji ya mafuriko hayo yakapita mbele ya nyumba na kumsomba.
Kuhusu wakazi wa mabondeni, Sadiki alisema kuwa baada ya mafuriko ya
2011, serikali iliwahamisha wananchi na kuwapatia viwanja Mbweni huku baadhi yao wakihama na
wengine wakigoma na kwenda mahakamani ambapo serikali ililazimika kutowahamisha kwa nguvu.
Hoja za wakazi hao kupingwa kuhamishwa ni kwa sababu wametumia gharama
kubwa katika ujenzi na kuwekewa huduma muhimu za maji na umeme, hivyo
hawawezi kuhama bila kufidiwa.
Mahakama tayari imetoa maamuzi
ya kuwataka wananchi kuhama huku serikali ikijipanga kutumia nguvu kuwahamisha tena bila kuwapatia maeneo mbadala.
Lakini kabla ya utekelezaji wa
zoezi hilo, mkuu huyo alieleza kuwa Mwenyezi mungu amepeleka mvua iliyosaidia na kutoa msaada kwa serikali kuwahamisha wananchi na kuipunguzia serikali kazi ya kuwahamisha kwa nguvu.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa baada ya usaidizi huu wa mvua kwa kuwahamisha
watu hao, sasa serikali imebakiwa kazi ndogo tuu ya kuhakikisha watu
hao hawarudi tena katika maeneo hayo na kuwasisitiza wale wote waliohama na
kubakiza baadhi ya vifaa vyao, mvua zikisimama wataruhusiwa kivichukua
kabla ya kupitisha tingatinga na kulisawazisha eneo lote kubaki
tambarare kama walivyofanya kwa eneo la Kipawa.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ameviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika
zoezi hili kuhakikisha wakazi wa mabondeni wanahama kwa ridhaa yao
kutekeleza amri ya mahakama na wale wote watakao kaidi, watahamishwa kwa
nguvu.http://www.jamiiforums.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMPONGEZA MWENYEZI MUNGU KWA KUSHUSHA MVUA ILIYOZAA MAFURIKO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment