BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHERIA YA MSWADA WA MAKOSA YA MTANDAONI YAPINGWA VIKALI MORO.

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akieleza jambo juu ya ukatili wanaofanyiwa waandishi wa habari ikiwemo tukio la yeye mwenyewe kufanyiwa ukatili wa kiwango cha juu hivi karibuni. PICHA/MTANDA BLOG.



Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (Misa-Tan), Simon akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani katika kilele chake iliyifanyika Mei 3 mwaka 2015 na kuandaliwa na MISA-TANZANIA hoteli ya Nashera Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Maggid Mjengwa mmiliki wa blog ya MJENGWA BLOG akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusiana na hekaheka za uandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyoadhimishwa kitaifa Morogoro chini ya MISA-TANZANIA.PICHA/MTANDA BLOG.
Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) Filiberto Sebregondi akisoma lisara wakati wa kilele hicho.


Mkurugenzi mkuu wa chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka kushoto akimweleza jambo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda. PICHA/MTANDA BLOG.
WAMILIKI WA BLOG, Juma Mtanda, wa kwanza kushoto chini ya MTANDA BLOG Maggid Mjengwa (katikati) wa MJENGWA BLOG na Joachim Mushi wa THEHABARI.COM wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani katika kilele chake Mei 3 mwaka 2015 iliyoandaliwa na MISA-TANZANIA hoteli ya Nashera Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi aliyekaa akizungumza jambo na Mratibu wa Club hiyo, Thadei Hafigwa.
PICHA/MTANDA BLOG.

WAMILIKI WA BLOG, Maggid Mjengwa wa MJENGWA BLOG kushoto, Juma Mtanda, wa kwanza kulia chini ya MTANDA BOG wakiwa na rafiki yao ambaye ni mdau wa habari kutoka UjerumanLi, Calaudia Depka (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo. PICHA/MTANDA BLOG.
 http://jumamtanda.blogspot.com/
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo, Assah Mwambene kushoto akiandika dondoo wakati Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena akizungumza jambo katika kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.PICHA/MTANDA BLOG.
Mkurugenzi mkuu wa chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka naye akizungumzia juu ya unyanyasaji wa kijinsia katika kongamano hilo, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura na katikati ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.PICHA/MTANDA BLOG.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (Misa-Tan), Simon Berege akisikiliza jambo kutoka kwa mwanachama wa Morogoro Press Club Halfan Diyu. PICHA/MTANDA BLOG.

HII NDIYO KERO MZINA IPO KATIKA VIFUNGU HIVI.
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).


2. Kifungu 21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale zitakapohitajika (kwa lazima).

3. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma)

4. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

5. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

6. Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa kiingereza “not less than”

7. Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

8. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

9. Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta status zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

10. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats n.k) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

11. Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states.

Askari Polisi wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua muda gani?

12. Kifungu 31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au Mtoa Huduma ya mtandao, pale unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka husika (Kama sheria inavyosema) askari naye anaweza kwa wakati huohuo akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako (kama sheria inavyosema), hivyo sheria inakinzana yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa kisheria.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: