BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MALARIA YAUA WATU 361 WAKIWEMO NA WATOTO ZAIDI YA 113 WILAYA YA MVOMERO MKOANI MOROGORO.

https://zanzibariyetu.files.wordpress.com/2013/06/latest-dengue-fever-in-lahore-punjab-dengue-report-updates2.jpg?w=584&h=371 

Mbu akinyonya damu kutoka kwenye mwili wa binadamu.

Juma Mtanda, Morogoro.
Halmashauri ya wilaya ya Mvomero imeanza mikakati ya kupunguza kwa kudhibiti maambukizi mapya ya Ugonjwa wa malaria baada ya watu 110,609 kukumbwa na ugonjwa huo na kusababisha vifo 361 kwa mwaka 2013 mkoani Morogoro.

 
Akizungumza na MTANDA BLOG wilayani humo, Mratibu wa Malaria wilaya ya Mvomero, Dk Wendy Munisi alisema kuwa kwa takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha kuwa watu 110,609 walikukumbwa na ugonjwa wa malaria na kusababisha vifo 361 wakiwemo watoto zaidi 113.
Dk Munisi alisema kuwa takwimu hizo ni kubwa hivyo Idara  ya afya Wilayani humo ipo katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali sambamba na kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo ili kuhakikisha wanapambana na kupunguza vifo vitakavyosababishwa na madhara ya maambukizi mapya ndani ya jamii.
“Kitu tunachopambana nacho kwa sasa ni kujikita kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kutokomeza mazalia ya mbu na kinga ya ugonjwa wa malaria katika ngazi ya familia na mtu mmoja mmoja ili kushusha idadi ya vifo na wagonjwa wanaoambukizwa ugonjwa malaria kwa mwaka hadi mwaka.”alisema Dk Munisi.
Dk Munisi alisema kwa mwaka huo 2013 jumla ya wagonjwa 110,609 walikumbwa na ugonjwa wa malaria kati yao 42,778 wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambapo wenye umri wa miaka mitano na kuendelea walikuwa 67,831.
Alisema kuwa wagonjwa 2,372 walilazwa katika vituo mbalimbali vya afya ambapo chini ya umri wa miaka mitano 1,118 , nao walilazwa wakati 1,902 wenye umri wa miaka mitano na kuendelea wakiingia katika orodha hiyo ya wagonjwa waliolazwa kutokana na ugonjwa huo wa malaria.
Alibainisha kuwa kati ya wagonjwa hao 110,609 waliougua malaria kwa mwaka huo 2013, 361 walifariki dunia huku watoto 113 wenye chini ya umri wa miaka mitano wakifariki dunia na wale wenye umri wa miaka mitano na kuendelea 62 walikufa kwa ugonjwa huo.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya afya ya Zahanati ya Dakawa, Gabriel Ngowi akizungumzia juhudi za sekta ya afya wilaya ya Mvomero kupunguza maambukizi mapya pamoja na vifo vinavyosaababishwa na ugonjwa alisema kuwa sekta ya afya inapaswa kuongeza juhudi za makusudi hasa kwa kujikita katika kutoa elimu ya namna ya kuangamiza mazalia ya mbu.
Ngowi alisema kuwa sekta ya afya inapaswa kujikita kwa kutoa elimu kwa wananchi ili kila mwananchi aweze kufahamu namna ya kudhibiti mazalia ya mbu na namna ya kujinga dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Aliyekuwa Mratibu wa kinga kupitia mradi wa hati punguzo kwa akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano wilayani humo, Khadija Kimwaga alisema kuwa wananchi sasa wanapaswa kuzingatia elimu zinazotolewa juu ya ugonjwa wa malaria na namna ya kujinga nao kutokana na ugonjwa huo kuwa tishio Wilayani humo.
Kimwaga alisema wananchi wakitumia vizuri elimu hiyo inayotolewa na wataalamu kutoka sekta ya afya itasaidia kupunguza vifo na maambukizi mapya ili wananchi waweze kuendelea vizuri na shughuli zao za maendeleo itakayosaidia kujenga uchumi wa nchi.CHANZO/MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: