Mama akifurahia jambo na mtoto wake, Picha ya Maktaba.
Mikingoti alisema matukio hayo yanaongezeka na kupungua katika vipindi tofauti. Alitolea mfano mwaka 2003, matukio 10 yaliripotiwa wakati 2004 yaliripotiwa saba.
“Mwaka 2006 yaliripotiwa matukio ya watu 36 kuuawa, huku mwaka 2010 ndiyo mwaka ambao matukio mengi zaidi yaliwahi kuripotiwa kwani watu 52 walipoteza maisha mikononi mwa polisi, mwaka 2013, watu 23 waliuawa kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili, mwaka 2014 takwimu za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola hazikupatikana,” alisema Mikongoti.
Jaji Mstaafu, Amir Manento akikata utepe kuzindua Taarifa ya Haki za
Binadamu ya Mwaka 2014, Dar es Salaam jana na kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen
Kijo-Bisimba.
Ripoti pia imebaini kuendelea kukithiri kwa matukio ya ubakaji. Mwaka 2008 kulikuwa na matukio 196, lakini mwaka 2014 kwa nusu mwaka pekee, matukio 3,074 yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi nchini.
Hata hivyo, Mikingoti alisema changamoto kwenye ubakaji bado ipo katika ukimya wa waathirika na jamii kwa ujumla. “Na hata wanaojitokeza kuyaripoti, bado hushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hizo.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Helen Kijo Bisimba alisema Serikali inapaswa kuhakikisha elimu ya haki za binadamu inatolewa kwa kina na kwa ngazi zote.
Alisema pia ihakikishe inawachukulia hatua kali wale wote wanaokiuka ili liwe fundisho kwa jamii inayowazunguka.
Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Harusi Miraj Mpatani alisema kwa upande wa Zanzibar, bado kuna upungufu mkubwa wa utekelezaji wa haki za msingi za binadamu.
Mikingoti alisema matukio hayo yanaongezeka na kupungua katika vipindi tofauti. Alitolea mfano mwaka 2003, matukio 10 yaliripotiwa wakati 2004 yaliripotiwa saba.
“Mwaka 2006 yaliripotiwa matukio ya watu 36 kuuawa, huku mwaka 2010 ndiyo mwaka ambao matukio mengi zaidi yaliwahi kuripotiwa kwani watu 52 walipoteza maisha mikononi mwa polisi, mwaka 2013, watu 23 waliuawa kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili, mwaka 2014 takwimu za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola hazikupatikana,” alisema Mikongoti.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Tanzania inaongoza barani Afrika kwa matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Toka mwaka 2008 mpaka 2010, jumla ya watu 75 waliuawa, ikimaanisha kwamba kila mwezi takriban watu watatu walikuwa wakiuawa.
Ripoti pia imebaini kuendelea kukithiri kwa matukio ya ubakaji. Mwaka 2008 kulikuwa na matukio 196, lakini mwaka 2014 kwa nusu mwaka pekee, matukio 3,074 yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi nchini.
Hata hivyo, Mikingoti alisema changamoto kwenye ubakaji bado ipo katika ukimya wa waathirika na jamii kwa ujumla. “Na hata wanaojitokeza kuyaripoti, bado hushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hizo.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Helen Kijo Bisimba alisema Serikali inapaswa kuhakikisha elimu ya haki za binadamu inatolewa kwa kina na kwa ngazi zote.
Alisema pia ihakikishe inawachukulia hatua kali wale wote wanaokiuka ili liwe fundisho kwa jamii inayowazunguka.
Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Harusi Miraj Mpatani alisema kwa upande wa Zanzibar, bado kuna upungufu mkubwa wa utekelezaji wa haki za msingi za binadamu.MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment