BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKIMBIZI WA BURUNDI 300 WAKUMBWA NA KIPINDUPINDU HUKU 30 WAKIFARIKI DUNIA KATIKA ARDHI YA TANZANIA.

 
Wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania.

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya visa 400 vya ugonja wa kipindupindu vinaripotiwa kila siku miongoni mwa wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania.

Maelfu ya watu wamewasili kwa mashua wakikimbia ghasia za kisiasa nchini Burundi

Wamechukua hifadhi katika sehemu zenye misongamano na zilizo na mazingira mabaya.

Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 3000 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu na hadi sasa zaidi ya 30 wameaga dunia.

Maandamano yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: