BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WATANO WAKUTWA NA VIUNGO VYA ALBINO WAKIUZA AKIWEMO MWALIMU WA SHULE YA MSINGI, HOTELINI SHINYANGA.

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limewakamata watu watano waliokuwa wamejificha katika hoteli moja iliyoko wilayani Kahama mkoani humo wakifanya biashara ya viungo vya binadamu vinavyodhaniwa kuwa nia vya albino hali ambayo inaonyesha dhahiri kuwa imani potofu na vitendo vya kishirikina bado vinaendelea kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha kukamatwa watu hao akiwemo mwalimu wa shule ya msingi Katunguru iliyoko katika tarafa ya msalala wilayani Kahama.


Mwalimu huyo ametambuliwa kwa jina la Bahati Kirungu huku kamanda Kamugisha akidai kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaojihusisha na biashara hiyo. ITV
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: