BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOKWEPA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) KUSAKWA UDI NA UVUMBA NA JESHI.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNWOe7lSOuCTsw5D8AKXJq-OkX6uRZl2z_3ByeOtnuYPVkTsOHtDq4MY4wdWo79NqDIH76d9KdmGt9yj541CeQt5c-KEmaSn29QyNHZofCJRDeX86WNzZQzhopF1ggtkB_aXP9lio7Afg/s1600/MAFUNZO.JPG

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa wakiwa tayari kwaajili ya Gwaride. PICHA YA MAKTABA.

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013/14, 2014/15 na kutojiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) bila ridhaa ya jeshi hilo, wanaendelea kusakwa na kuorodheshwa kwenye orodha ya watoro na upo uwezekano wa wao kwenda mafunzo hayo mapema mwezi ujao.


Akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo bungeni jana ya Makadiro ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2015/16, Dk Mwinyi alisema mafunzo ya JKT kwa wahitimu hao hutolewa kwa mujibu wa Sheria, ambapo ni ya kuwajengea uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kutoa stadi za kazi.

Alisema kwa mwaka 2014/15 jumla ya vijana waliopata mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria ni 31,635 ambayo ni sawa na ongezeko la vijana 15,632, ukilinganisha na vijana 16,003 waliohitimu mafunzo hayo mwaka 2013/14 .
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgJWTa46EqLDHXQFALtYfEtwrZ9CWDqUm_XR0NIl3lgNNKm48scqfhwO8Mv1zovd9gl0iZlkBfB7b2ODhsAScEbBSePm2STWulJ70mLf07EnlAhMJRLnpGkqeccYRP2lTTWLecUz84mWtM/s1600/unnamed+(74).jpgWAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

 “Hata hivyo idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na idadi ya vijana 41,000 waliohitimu kidato cha sita, waliostahili kujiunga na mafunzo hayo, na sababu zilizofanya upungufu huo ni pamoja na kalenda ya awamu ya pili ya mafunzo kugongana na kalenda ya kuanza mihula ya masomo ya elimu ya juu”, alisema Dk Mwinyi.

Na kuongeza vijana waliopaswa kujiunga na mafunzo hayo ila hawakujiunga bila ridhaa ya jeshi, wameingizwa kwenye orodha ya watoro wa jeshi hilo na kwamba wizara inaangalia uwezekano wa kuiwezesha JKT, kuchukua kundi hilo wakiwemo watoro, kuanza kwa mkupuo mmoja mafunzo hayo Juni hadi Agosti mwaka huu.

“Tunatafuta uwezekano wa kuiwezesha JKT, kuwachukua watoro wa mafunzo hayo na wale walioshindwa kujiunga kwa kugongana kwa mihula ya masomo, kuingia mafunzoni kwa mkupuo mmoja kuanzia mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu, ili wawahi muhula wa masomo kwa elimu ya juu”, alisema Dk Mwinyi.

Hivyo aliwataka vijana wote waliohitimu kidato cha sita na kupaswa kujiunga na JKT, na hawakufanya hivyo bila sababu wala kupata ridhaa ya jeshi hilo wafahamu wako kwenye orodha ya watoro wa jeshi hilo na kwamba ni lazima watapaswa kwenda mafunzoni.

Akizungumzia changamoto zinazokabili utekelezaji wa mafunzo hayo hivi sasa, Dk Mwinyi alisema ufinyu wa bajeti unasababisha mafunzo hayo kushindwa kutelekezwa kwa sasa, kwani kuna uhaba wa fedha za kugharamia huduma za mafunzo pamoja na kushindwa kukarabati majengo ya miundombinu katika makambi ya jeshi.

Na kufafanua kuwa fedha zinazotolewa ni kidogo na zinaifanya JKT kuwa kwenye madeni makubwa na kuishauri serikali itoe fedha za kuwawezesha kumaliza ukarabati wa kambi zao ili waweze kuwachukua wahitimu wote wa kidato cha sita kwa mkupuo mmoja, utakaowezesha kumaliza mafunzo mapema na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa wakati.

Alisema ufinyu huo wa bajeti umefanya pia miradi ya maendeleo kushindwa kutekelezwa kama bajeti ilivyopitishwa ambapo hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2014/15 fedha zilizopokewa na wizara hiyo zilikuwa asilimia 29.5 ya bajeti iliyoidhinishwa.

Na kufafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2014/15 wizara iliomba Sh bilioni 708.7 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo lakini hadi kufikia Machi mwaka huu,fedha zilizoidhinishwa ni Sh bilioni 248.8 ikiwa ni sawa na asilimia 35.1 ya mahitaji halisi.

Kwa mwaka wa fedha 2015/16, Wizara hiyo inaomba kuidhinishiwa jumla ya Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: