BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BADOBODA 15 WASWEKWA LUPANGO BAADA YA VURUGU ZA KUPINGA MWENZAO KUKAMATWA KISHA KUMSHIKA MAKALIO ASKARI WA ZIMAMOTO

Juma Mtanda na Pascalina Kidyalla, Morogoro.
Watu 15 zikiwemo pikipiki tano zinashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi kufuatia vurugu iliyohusisha waendesha pikipiki za biashara (bodaboda) na askari polisi kutokana na kuwepo kwa tuhuma za mwendesha pikipiki mmoja kudaiwa kumshika makalio askari wa kike wa jeshi la Zimamoto na Ukoaji Manispaa ya Morogoroo.


Vurugu hizo zilitokea baada ya dereva huyo aliyefahamika kwa jina la Juma Abdallah kufanya shambulio la aibu kwa askari aliyekuwa akielekea kazini majira ya saa 3 asubuhi Juni 10 mwaka huu.

Akizungumza na waandishii wa habari eneo la tukio, Afisa habari wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji kituo cha Fire, Issa Isandekeku alisema kuwa jana (juzi) majira ya saa 3 asubuhi askari wa jeshi hilo (jina limehifadhiwa) alishambuliwa kwa tukio la aibu na dereva wa bodaboda kisha kukimbia baada ya kufanya tukio hilo.

Isandekeku ambaye ni mkaguzi msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji hilo alisema jana kuwa mtuhumiwa alishikwa na askari wa jeshi hlo lakini baadaye kulizuka vurugu zilizoanzishwa na waendesha pikipiki wakipinga mwenzao kukamatwa.


Katika vurugu hizo waendeshapikipiki walifunga barabara na kurundika mawe na takangumu barabara ya Mindu kata ya Kingo na kusababisha shughuli mbalimbali ikiwemo maduka kusimama kwa zaidi ya saa 1:30.

"Hizi vurugu zimesababishwa na waendesha pikipiki kwa kuzuia barabara ya Mindu isitume baada ya kuweka vizuiwi barabarni kwa kuweka mawe na taka ngumu, mwenzao amekatwa kufuatia kumfanyia tendo la udhalilishaji askari wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji akiwa na sare kinyume na sheria za nchi."alisema Isendekeku

Isendekeku alisema baada ya jeshi la Zimamoto kuzidiwa nguvu walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kudhibiti hali hiyo na kufanya eneo hilo kurejea kwa utuli u wake.

Katika vurugu hizo askari wa jeshi la polisi, Rajabu Seleman aliyeruhiwa kichwani kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali wakati wa kutuliza vurugu hizo.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi, Mussa Maramba kutokana na vurugu hizo watu 15 wamekamatwa pamoja na pikipiki tano zilizotelekezwa na waendesha bodaboda hao baada ya vurugu hizo.

Kamanda Maramba alisema kuwa watu hao watafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa upelelezi na kutoa wito kwa wananchi kuwa watulivu wakati askati anapotekeleza majukumu yake ya kazi.

"Vurugu hizi ukiangalia hazikuwa na sababu ya msingi ya kufanya vurugu kwani tayari mtuhumiwa amekamatwa unafanya fujo kwa maslahi ya nani ?".alihoji.

Jeshi la polisi walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatanya vijana waliokuwa wanafanya vurugu na kuweka taka ngumu barabarani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: