Askari saba wa Jeshi la Polisi nchini, kitengo cha Usalama Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali iliyohusisha gari la Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.
Ni baada ya dereva kusimamishwa na kukataa, Trafiki wakapiga simu mbele, alipofika akakuta askari wameweka kizuizi njiani akawagonga.
Taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa na jeshi hilo zinaelewa kuwa watu watatu wamefariki hapo hapo.
Gari zilizohusika katika ajali hiyo, zote ni aina ya Toyota Land Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la Polisi nchini, na jingine lenye namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya kampuni moja ya Utalii mkoani humo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kupitia taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa kijamii unaoendeshwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo imesomeka kama ifuatavyo.
Ni kweli ajali imetokea na kusababisha majeruhi 7 wakiwa ni askari wa Usalama barabarani Arusha. Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva hatimaye kushindwa kumudu gari na kusababisha gari kuhama njia na kugonga gari la Polisi lililokuwa linakuja mjini Arusha.
Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospita kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea vizuri.
chanzo: http://www.jamiiforums.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ BREAKING NEWS ! ASKARI SABA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARA WAPATA AJALI, WATATU WADAIWA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO ARUSHA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment