BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EDWARD LOWASSA AJIFANANISHA NA WASHAMBULIAJI WA MCHEZO WA SOKA CHRISTIAN RONALDO NA LION MESSI, NJIA YA KUINGIA IKULU SASA NYEUPE.

 
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amezidi kupata maelfu ya wanachama wa CCM kumdhamini huku akisema kutokana na wingi wa watu wanaojitokeza tayari ameshafunga magoli ya urais.


Lowassa aliwasili jana katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea Tanga na kupata wadhamini 33,780 katika mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi, Lowassa alisema anajivunia rekodi yake kwa Watanzania kutokana na kumjua na kujua nguvu yake katika utendaji kazi.

“Nadhani wale wenzangu 36 wakiona umati huu watajua na kujionea kuwa nimeshafunga magoli, tena magoli yenyewe ni sawa na yanayofungwa na Ronaldo (Cristian) na Messi (Lionel) hayana ubishi,” alisema Lowassa.

Alisema nia yake ya kugombea urais ni kutokana na kujiamini, ana uwezo, anatosha na amegombea ili ateuliwe na Chama hicho aweze kupambana na umaskini katika Taifa lenye rasilimali nyingi.

Akitangaza idadi ya watu waliojitokeza kumdhamini Lowassa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Cyril Chami, alisema Lowassa amepata wadhamini 33,780 katika mkoa huo.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani humo, Vick Nsilo Swai, alisema akinamama wa mkoa huo watahakikisha anashinda katika safari yake ya matumaini kutokana na utendaji aliouonyesha. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: