BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIONGOZI MKUU WA ACT-WAZALENDO ZITTO KABWE AJIGAWIA JIMBO LA CCM CHINI YA MBUNGE PETER SERUKAMBA KIGOMA.

http://api.ning.com/files/3vKQkh-FlonUo2oD0ORv4ai1lWb099aOAJqsLzaguTBQxI7dQFD42em*D4ucFl1PX1oBBTI4y53ns*2U-uMUOSIhD-Ph-PCB/ZITTOKABWETABORA1.jpg 
Kigoma. Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anakusudia kuwa mbunge wa Kigoma Mjini kwa kipindi kimoja cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2020, kabla ya kuomba kazi nyingine ya kufanya kwa Watanzania. Mbunge wa Jimbo hilo kwa sasa ni Peter Serukamba wa Chama cha Mapinduzi (CCM).


Akizungumza baada ya kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura katika Kituo cha OTTU Mwanga Mjini Kigoma juzi, Zitto alisema ana dhamira ya kuhakikisha ACT inashinda majimbo yote manane katika Uchaguzi Mkuu mkoani hapa.


“Tumejipanga vizuri kushinda majimbo yote ya Mkoa wa Kigoma, lakini tuna uhakika wa kupata nusu ya majimbo mkoani Tabora na lazima tupate majimbo yote ya Kahama. Tumejipanga vizuri kushinda bila shaka baada ya Oktoba 25 watu watajua hiki tunachokisema leo,” alisema Zitto.


Alisema baada ya kuhakikisha Kigoma Mjini inanufaika na miradi ya barabara, Uwanja cha Ndege, ujenzi wa Bandari kavu ya Katosho na Kibirizi wakati huo akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa sasa anakusudia kupigania upatikanaji wa umeme wa maji kutoka Mto Malagarasi.


“Kigoma ni mji wa biashara, lazima eneo la Bandari ya Kigoma liwe la kimkakati kwa sababu tunakusudia kuifanya Kigoma kuwa eneo maalumu la biashara kwa ukanda huu wa Maziwa Makuu, mikakati imeandaliwa tayari.


“Lakini hili litafanikiwa ikiwa tutapata umeme wa uhakika badala ya huu wa kutegemea mafuta ambao ni ghali kuuendesha,” alisema.


Kuhusu gharama kubwa ya umeme, Zitto alisema: “Kila mwezi Tanesco wanatumia Sh2 bilioni kuzalisha umeme Kigoma lakini wanakusanya Sh300 milioni kwa mwezi, sawa na robo ya gharama halisi za uendeshaji, lazima tupiganie umeme wa Malagarasi utakaozalisha megawati 48 zitakazowezesha kuendesha viwanda vikubwa na vidogo vya kuzalisha na kuchakata mazao mbalimbali.”


Hata hivyo, Zitto hakutaka kuzungumzia kwa undani maelezo yake kwamba atakuwa mbunge kwa kipindi kimoja ili itakapofika 2020 aombe kazi nyingine kwa Watanzania.


Zitto huku akicheka alijibu: “Tusubiri kwanza watu wachukue fomu za kugombea urais, haya mengine tutazungumza tu kwani muda bado upo, lakini nitawaomba Watanzania wanipe kazi nyingine niwatumikie.”


Katibu wa ACT Wilaya ya Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema kuna changamoto zinazowakabili hususan ugumu wa baadhi ya watu kuandikishwa kutokana na wingi wao na uchache wa mashine. Alisema watu wengi wamekata tamaa na wameamua kususia kazi hiyo.


Mkazi wa Kisangani Mwanga, mjini Kigoma, Monica Abel alisema ujio wa Zitto utaongeza ushindani kwa wagombea kutoka vyama vingine na kuwataka watu kujitokeza kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: