Na Juam Mtanda, Morogoro.
Wadau wa ardhi mkoa wa Morogoro wameibua sababu mbalimbali zinazochangia na kuzalisha migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji kuwa yanatokana na makundi ya wawekezaji wa makampuni ya kigeni ikiwemo na udhaifu wa mifumo ya kisheria na kiutawala hapa nchini.
Akizungumza wakati wa mdaharo wa mkoani hapa, Mhadhiri wa chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro Paul Mtoni wakati wa mdaharo wa haki za ardhi alisema kuwa chanzo cha kuzaliwa kwa migogoro ya ardhi kunatokana na udhaifu wa mifumo ya kisheria na kiutawala sambamba na makundi ya wawekezaji wa makampuni ya kigeni kuhodhi ardhi kubwa bila kuitumia.
Mtoni alisema kuwa endapo serikali ingedhibiti baadhi ya makundi ya wawekezaji wa makampuni ya kigeni, kuangalia upya udhaifu wa mifumo ya kisheria na kiutawala hapa nchini, migogoro mingi ya ardhi ingekuwa tayari imepatiwa ufumbuzi tofauti na sasa ardhi kubwa inamilikiwa na wawekezaji ambao baadhi yao hawaitumii.
“Huu mdaharo wa haki za ardhi na kuangalia namna ya kutatua wake migogoro ya ardhi haki Tanzania umekuja wakati muafaka lakini serikali kiujumla wake inapaswa kuangalia upya hawa wawekezaji wa makampuni ya kigeni na kuangalia kwa jicho la upande wa pili udhaifu wa mifumo ya kisheria na kiutawala ambao unachangia kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi.”alisema Mtano.
Nina imani kubwa migogoro ya ardhi Tanzania inaweza kuisha endapo tu serikali itajipanga kuanzia ngazi ya taifa na kushuka hadi ngazi ya chini ikiwemo vijiji na vitongoji kuweka mikakati kuangalia mashamba yaliyotelekezwa bila kutumika kwa miaka mingi ili kuweza kupewa wananchi kutumia katika shughuli mbalimbali.alisema Mtoni.
Kwa upande wa ufugaji, Mason Lemameo mkazi wa Msowelo wilaya ya Kilosa, alisema kuwa matatizo ya ardhi na migogoro yake kwa Tanzania yamekuwa sugu kutokana na baadhi ya wafugaji wageni kuvamia ardhi kwa ajili ya malisho jambo linalowaingiza katika migogoro na wakulima.
Naye Mratibu wa mtandao wa haki za ardhi mkoa wa Morogoro, Mohamed Mapalala alisema kuwa mkoa huo ni mikoa yenye migogoro mingi ya ardhi kutokana na kuwa na ardhi mzuri yenye rutuba na kuwavutia wafugaji kulisha mifugo sambamba na shughuli za kilimo.
Mapalala alisema kuwa kutokana na ardhi ya Morogoro kuwa na rutuba mzuri ya kustawisha mimeo ya mbalimbali ya chakula na malisho ya mifugo kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara inayozalishwa inayopelekea jamii hizo kuishi kiuhasama na kupelekea mapigo yanayosababisha vifo, majeruhi na vilema vya kudumu.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment