Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewaeleza watanzania kuwa endapo CCM itampitisha na kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao na kushinda nafasi hiyo jambo la kwanza ni kufufua viwanda na kujenga viwanda vipya ili kuweza kuzalisha ajira za kutosha.
Membe atakuwa mkali katika kukataza viongozi kujihusisha katika ulaji rushwa huku akibainisha baadhi ya vipaumbele kuwa Tanzania kuwa na utawalam bora na uchumi wa viwanda.
Akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Morogoro mtaa wa Makongoro mjini hapa leo mara baada ya kukabidhiwa fomu za wadhamini 950, Membe alisema kuwa kamati kuu ya CCM haitakuwa imefanya makosa wala kujuta endapo itamteua kupeperusha bendera ya CCM huku akiwa na lengo kuu kuzalisha ajira kwa vijana kwa kufufua viwanda vilivyokufa sambamba na kujenga vipya.
Membe alisema kuwa Tanzania ina nishati nyingi ikiwemo ya gesi na umeme wa upepo kuwa nishati hiyo itatosha kuendesha viwanda huku akiwekea mkazo katika suala la kilimo kikiwemo cha pamba na mazao mengine ya biashara.
“Kuna mambo ya msingi endapo chama kitaniteua kuwa mgombea urais na kushinda uchaguzi mkuu ujao, dhamila yangu ni kuinua uchumi kwa kufufua viwanda vilivyokufa lakini na kujenga vipya ili kuzalisha ajira za kutosha kwa watanzania na kuweka mkazo katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara.”alisema Membe.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kazi hiyo suala la Tanzania kuagiza mitumba kutoka nje ya nchi itakuwa historia kwani viwanda hivyo vitajitoshereza kukidhi mahitaji ya watanzania.
Vitu kama baiskeli, magari na vyombo vingine viwanda hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha na bidhaa nyingine.
Tanzania itakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa zilizosindikwa kwa bei nafuu na kuuza kwa bei kubwa nchi za nje na kuongeza kipato cha taifa.
Akizungumzia upande wa namna anatavyopamba na wala rushwa, Membe alisema kuwa kazi kubwa atayokuwa nayo ni kurekebisha sheria ya makosa ya rushwa kwanza ili kuweza kuwashughulikia vilivyo mapapa wala rusha.
“Nitapambana kwanza na wala rushwa wakubwa (mapapa) isipokuwa mtoa rushwa ndiye atakuwa wa kwanza kushughulikiwa na endapo mpokeaji atatoa taarifa kabla hiyo itakuwa manusura yake.”alisema Membe.
Aliongeza kwa kusema atapelekwa mahakamani kama sheria inavyotaka lakini kama ushahidi haujatoshereza kitachofuata hapo ni kumfukuza kazi endapo mtumishi huyo ni waserikali au chama.
Kwa upande mwingine Membe aliwapiga kijembe wagombea wenzake katika nafasi hiyo kwa kuwataka kukubali matokeo ya kamati kuu ya CCM endapo mtu hatakidhi vigezo na kukatwa jina lake itamlazimu kukaa kimpya.
Kamati kuu imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanzishwa kwake na kufanya hizi kazi na kuwataka wajumbe wa kamati kuu kutotishwa na mtu ama kikundi chochote kwani CCM ndiyo chama kikubwa kuliko mtu au fedha.
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Morogoro, Kulwa Milonge alimweleza Bernard Membe kuwa, wamejitokeza wanaCCM 950 kumdhamini huku mwenyewe akiwa na mahitaji ya wadhamini 450 na kuwashukuru walionyesha nia ya kumdhamini.
0 comments:
Post a Comment